27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kasi ya ongezeko la watu tishio Geita

Na Yohana Paul, Geita

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) limeutaja mkoa wa Geita kama eneo lenye kasi kubwa ya ongezeko la watu nchini Tanzania hali inayohitaji hatua thabiti kufikia maendeleo endelevu.

Mchambuzi wa Idadi ya Watu na Maendeleo kutoka UNFPA, Ramadhani Hangwa amebainisha hayo mjini Geita alipobainisha kuelekeza maadhimisho ya siku ya idadi ya watu nchini yanayofanyika Geita.

Hangwa amesema mkoa wa Geita una watu takribani milioni 2.9 kati ya watu milioni 61 wa nchi nzima ambapo kasi ya ongezeko la watu kitaifa ni asilimia 3.2 huku kwa mkoa wa Geita ni asilimia 5.4.

“Pia wastani wa watoto ambao mwanamke anaweza kuwa nao kitaifa ni watoto wanne lakini kwa mkoa wa Geita wastani wa watoto ni sita.”

Ameongeza kuwa takwimu za kitaifa zinaonyesha kwamba asilimia 11.2 ya idadi ya watu kati ya ile milioni 61 wana aina moja au zaidi ya ulemavu kwa mkoa wa Geita ambao ni asilimia 10.2.

“Kwa hiyo siku ya idadi ya watu duniani tumeileta Geita kwa mikakati maalum baada ya kuonekana kwamba Geita kuna hizi Changamoto.”

Ofisa Mipango kutoka Tume ya Mipango Zanzibar, Umrat Suleman amesema maadhimisho hayo yanahusisha taasisi za umma na binafsi kufikia utatuzi wa changamoto za kijamii.

Amedokeza kuwa takwimu za afya ya uzazi pia kwa mkoa wa Geita zimeonekana zipo juu na hivo kuelekea maadhimisho haya yataangazia namna bora ya kumaliza ama kupunguza tatizo.

Mkuu wa Uchechemuzi wa Shirika la Marie Stops Tanzania, Oscar Kimaro amesema wanashirikiana na serikali kufanikisha adhima ya maendeleo endelevu yanayoendana na idadai ya watu nchini.

“Katika tafsiri ya kawaida kwa takwmu hizo, imekuwa ni ngumu sana kwa serikali kutoa huduma za maendeo zinazohusu afya na huduma mbalimbali za kijamii,”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles