26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania imepiga hatua katika usambazaji wa umeme vijijini-Dk. Kikwete

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Tanzania imepiga hatua kubwa katika usambazaji wa nishati ya umeme vijijini, kutoka asilimia 10 mwaka 2005 hadi kufikia zaidi ya asilimia 90, hatua iliyotajwa kama maendeleo ya kupigiwa mfano.

Hayo yamebainishwa Jumamosi, Julai 6, 2024, na Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete, alipotembelea Banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika Maonyesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Dk. Kikwete alisema wakati anaingia madarakani, vijiji vilivyokuwa na umeme vilikuwa asilimia 10 tu, lakini hadi sasa vijiji vilivyokwisha unganishwa na nishati hiyo muhimu ni 12,031 kati ya vijiji 12,318 vya Tanzania.

“Umeme ni kichocheo kikubwa cha maendeleo,” alisema Dk. Kikwete. “Kupitia REA, tunagharamia umeme kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuwafikia wananchi vijijini kwa gharama ya shilingi 2,700, TANESCO ni wafanyabiashara.”

Dk. Kikwete alieleza kuwa wakati anapokea uongozi kutoka kwa Hayati Benjamin Mkapa, matumizi ya umeme nchini yalikuwa asilimia 10. “Tulifanya kazi ya kuongeza matumizi ya umeme, na mpango wa REA ulianzia kwa Hayati Mkapa, mimi nilitimiza na kuzindua,” alisema.

Aliongeza kuwa, kwa sasa, asilimia kubwa ya vijiji vina umeme, na REA imefanya kazi kubwa kuhakikisha vijijini wanapata umeme. “Bila ya umeme hakuna maendeleo,” alisema Dk. Kikwete.

Dk. Kikwete alisema kuwa wakipata umeme, watu wa vijijini wataweza kuwa na mashine za kusaga na kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo. “Kipindi changu nilikuwa na wazo la kupunguza matumizi ya mkaa, tupande miti na kupunguza matumizi ya mkaa. Gharama ya umeme ilivyopanda, wakarudie waangalie gharama,” alisema.

Alisisitiza umuhimu wa kuangalia namna ya kupunguza gharama ya gesi na umeme ili watu wasirudi kwenye matumizi ya mkaa.

“Tuangalie namna ya kupunguza gharama ya gesi na umeme ili watu wasirudi kwenye matumizi ya mkaa,” alihitimisha Dk. Kikwete.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles