Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
BODI ya Sukari nchini Tanzania imesema msimamo wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuwalinda wananchi, wakulima, wawekezaji na wadau wengine muhimu kwa kuhakikisha inafanya maboresho makubwa kwa maslahi ya Watanzanaia wote.
Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Tanzania, Profesa Kenneth Bengesi, aliwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni siku chache baada ya kupitishwa sheria mpya ya sukari nchini.
“Tunaendeleza majadiliano na wadau ili kutatua changamoto zote sambamba na kuikuza sekta ya sukari kwa sababu ni jambo nyeti na muhimu, hivyo tunalichukulia hili kwa umakini,” amesema Profesa Bengesi.
Kwa siku za karibuni kumekuwa na mijadala kadhaa kutokana na siku chache zilizopita kugubikwa na uhaba wa sukari hali iliyoibua hofu kwa Watanzania wote.