24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mchuano mkali siku ya kwanza Vodacom Lugalo Open

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Shindano la wazi la mchezo wa gofu ‘Vodacom Lugalo Open 2024’, limeanza kwa kishindo  leo Julai 5, 2024 kutokana na wachezaji kujitokeza kwa wingi kushiriki michuano hiyo, hali inayoongeza ushindani.

Ikiwa ni siku ya kwanza ya shindano hilo  linalofanyika katika viwanja vya Klabu ya Gofu Lugalo, jijini Dar es Salaam, likihusisha wachezaji wa ridhaa na kulipwa, mchuano umekuwa mkali kila mchezaji akihitaji kuibuka kinara.

Akizungumzia shindano hilo, Nahodha wa klabu ya Lugalo, Meja Japhet Masai amesema wanatarajia ushindani kuongezeka katika siku ya pili na tatu kutokana na hali ilivyoanza.

“Tumefanikiwa kwa siku ya kwanza, shindano limekwenda vizuri na wachezaji wote waliojiandikisha wamejitokeza kwa wakati,” ameeleza Meja Masai.

Naye Jumanne Mbunda wa klabu ya  Lugalo  aliyeongoza kwa siku ya kwanza kwa mikwaju 74,amesema amecheza vizuri kutokana na hali ya viwanja na matarajio yake ni kuibuka kinara.

Mchezaji mwingine wa Lugalo, Isihaka Daudi amesema amefurahishwa na kiwango chake cha leo licha kwamba ameanza tofauti na alivyotarajia lakini anatarajia kuaongeza nguvu siku inayofuata.

“Kila mtu ana ari ya kufanya vizuri lakini matokeo ya Jumapili kila mtu atajua, nimefanya makosa kwa leo ila nitajitahidi kurekebisha,” amesema mshiriki Hawa Wanyeche.

Kwa upande wake Nuru  Morel wa  Arusha Gymkhana aliyeanza kwa mikwaju 73 amewatahadharisha wapinzani wake kwa kusema ametoka Arusha  kuja kushindana.

Klabu zinazoshiriki ni Arusha Gymkhana,Dar Gymkhna, Morogoro Gymkhana, Moshi,TPC Moshi, Mufindi Golf Nawenyeji Lugalo.

.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles