28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yazidi kutengeneza mazingira wezeshi ya uwekezaji kiuchumi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama amesema uwepo wa Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati na Uwekezaji ni maono na maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ni mipango inayoendana na Dira ya Taifa.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama alipowasili katika Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati na Uwekezaji.

Waziri amesema hayo leo Aprili 28,2024 jijini Dar es salaam wakati akimkaribisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko Kufunga Kongamano hilo lililoandaliwa na Baraza la Uwekezaji wa Wananchi Kiuchumi (NEEC).

Waziri alieleza kuwa Serikali itaendelea kutengeneza mazingira wezeshi kwa Watanzania ili kupata fursa ya kushiriki katika shughuli za kiuchumi, kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na kutengeneza uchumi jumuishi utakao inua uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama kabla ya kufunga Kongamano la Kitaifa Nne la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati na Uwekezaji jijini Dar es Salaam.

“Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa mfano wa kuigwa kwa hekima na busara katika kufanya mamuzi ndani ya Serikali yanayojumuisha makundi yote, na jambo hili tunalolifanya linaakisi maono yake ya falsafa ya R4,” amesema Waziri Mhagama.

Aidha, akieleza kuhusu Mkutano huo alisema unatija kubwa kwa ustawi wa taifa na kusisitiza kuwa utaendelea kuitishwa ili kuhamasisha, kuhimiza na kujenga uelewa wa pamoja ili kuongeza nguvu katika suala zima la uwekezaji.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama akizunguma jambo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Anderson Mutatembwa wakati wa Kongamano la Nne Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati na Uwekezaji.
Matukio katika picha baadhi ya Washiriki waliohudhuria Kongamano la Nne la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati na uwekezaji wakiwa uhairishaji wa Kongamano la kitaifa la ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati na Uwekezaji.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles