28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Tabora iko nyuma kielimu, vyoo bora

Na Sabina Wandiba, Mtanzania Digital

Mkoa wa Tabora umetajwa kuwa nyuma Kitaifa kwa watu wanaojua kusoma na kuandika ikilinganishwa na mikoa mingine nchini huku Dar es Salaama ikiwa kinara kwa watu wanaojua kusoma na kuandika.

Taarifa hiyo imetolewa Machi 14, 2024 jijini Dar es Salaam na Mtakwimu Mwandamizi Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Omary Mdaka, wakati akiwasilisha mada katika Mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusiana Usambazaji na Uhamasishaji wa Matumizi ya matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka 2022.

Mdaka amesema kuwa, katika zoezi hilo la ukusanyaji takwimu mbali mbali, pia imebainika kuwa, kwa upande wa elimu, Mkoa wa Tabora ndo upo nyuma kwa idadi ya watu wanaojua kusoma na kuandika kwa kiwango cha asilimia 68.0 ukilinganisha na mikoa mingine hapa nchini.

“Imebainika wananchi wengi wa Tabora hawajui kusoma na kuandika na hii itasaidia kufanya utafiti zaidi kujua sababu hasa zinazopelekea mkoa huo kuwa nyuma kwa kiasi hiki,” amesema Mdaka.

Aliongeza kuwa, katika takwimu hizo Mkoa wa Dar es Salaam ndo unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaojua kusoma na kuandika kwa asilimia 97.5.

Aidha, ameongeza kuwa, kwa upande wa matumizi ya vyoo bora, Mkoa wa Kagera ndio upo nyuma kwa wanaotumia vyoo bora kwa asilimia 32.2 ikifuatiwa na Mkoa wa Simiyu ambao wanaotumia vyoo bora ni asilimia 32.5.

Amesema, hii inaonyesha kuwa, wakazi wengi wa mkoa huo hawatumii vyoo bora na wengi wanajisaidia maporini na mtoni.

Ameutaja Mkoa wa Dar es Salaam kuongoza kwa matumizi ya vyoo bora kwa asilimia kwa asilimia 97.7.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles