25 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Rukwa kuanza kutumia umeme wa Gridi

Na Mwandishi wetu,Dodoma

Serikali imeanza kutekeleza mradi wa kupeleka umeme wa Gridi katika Mkoa wa Rukwa kupitia mradi wa TAZA, ulioanza kutekelezwa Novemba, mwaka 2023 na unatarajiwa kukamilika Agosti, mwaka 2026.

Hayo yameelezwa leo bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga wakati akijibu swali la Mbunge wa Nkasi, Aida Khenani aliyetaka kufahamu mkakati wa kumaliza changamoto ya upatikanaji umeme wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa.

Amesema kuwa, kwa sasa TANESCO inaendelea kufanya maboresho ya miundombinu ili kupunguza changamoto ya upatikanaji umeme mkoani humo na kujenga kituo kipya cha kupoza umeme.

Kuhusu hali ya upatikanaji umeme nchini amesema kuwa tatizo la upungufu wa umeme linaendelea kupungua, akitaja takwimu kuwa, umepungua kutoka megawati 400 hadi 144 kwa siku ya jana.

Ameeleza kuwa, Serikali inaendelea kufanya juhudi mbalimbali ili kuboresha hali ya upatikanaji umeme nchini akitolea mfano utekelezaji wa Mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) ambao inatarajiwa kuwa, katika mwezi wa Pili kuelekea Machi mwaka huu utaanza kuingiza megawati 235 katika Gridi ya Taifa.

Kapinga pia amezungumzia kazi ya upelekaji umeme wa Gridi mkoani Katavi ambapo ameeleza kuwa, tayari kuna mradi unaoendelea kutekelezwa na kwa sasa baadhi ya vituo vya kupoza umeme vimekamilika na hivyo, nguvu sasa inawekwa zaidi katika ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kwenda mkoani humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles