25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

MNEC Simiyu atimiza ahadi aliyoitoa mbele ya Makonda

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Mkoa wa Simiyu (MNEC), Emmanuel Gungu Silanga ametimiza ahadi yake aliyoitoa mbele ya Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Paul Makonda ya kununua baiskeli kwa mtu mwenye ulemavu ambaye aliomba msaada huo katika ziara ya mwenezi huyo katika Kata ya Lamadi wakati akielekea mkoani Mara.

Akizungumza na mabalozi wa CCM, katika Kata ya Lamadi mkoani Simiyu alipofika kwa lengo la kukabidhi msada huo, Gungu alisema katika ziara hiyo ya Mwenezi wa Taifa walijitokeza watu wengi kuomba misaada na walisaidiwa hapo hapo.

“Katika ziara ya Mwenezi Makonda wakati anaelekea Mkoani Mara kwenye ziara yake ya kikazi kama mnakumbuka kuna mwenzetu mmoja alijitokeza nakuomba msaada wa Baiskeli ili kumuwezesha kufanya shughuli zake, mimi nilisema nitampa na leo Januari 28, 2024 nimeileta kuikabidhi,”alisema Gungu.

Aidha, Gungu amewataka mabalozi wa CCM kuchapa kazi, kwani chama kinatambua kazi kubwa wanazofanya na kwamba ataketi nao pamoja baada ya mabalozi wa jimbo la Busega kumuomba wakae nae kwani wanamambo mengi ya kumwambia.

Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Busega, Kauli Mayala alimshukuru Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu CCM Taifa kwa kutimiza ahadi yake na kueleza kuwa Baiskeli hiyo itamfikia mlengwa mara moja.

“Tunakushukuru sana Mheshimiwa Mnec kwa moyo wako wa upendo katika ziara ya Mwenezi wetu wa Taifa Makonda uliahidi hapa Lamadi na umetekelza. Leo kwa furaha tunapokea Baiskeli hii nikuhakikishie itamfikia muhusika mara moja,” alisema Mayala.

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Anna Gidarya alimakabidhi Baskeli Mlemavu huyo, John Charles kwa niaba ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Emmanuel Gungu Silanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles