27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Tanzania, Cuba zasaini makubaliano kuboresha sekta ya afya, elimu

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Serikali ya Tanzania na Cuba zimesaini hati za makubaliano mbili na kukubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano wao zaidi katika sekta ya afya, elimu, kilimo na kuendelea kuboresha uhusiano wa siasa na uchumi.

Hati hizo ni makubaliano ya Chuo Cha Artemisia Dius Gonzales Cha Cuba na Chuo Cha Kilimo Cha Sokoine na hati ya makubaliano kati ya Center for State Control of Medicines and Medicine Divices(CECMED) ya Serikali ya Cuba na Mamlaka ya Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) katika kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya kiwanda cha viuatilifu vya maralia kilichopo Kibaha na kuzalisha dawa nyingi za binadamu na wadudu.

Akizungumza jana Januari 24 Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kushudia kusainiwa hati hizo,Makamu wa Rais Tanzania, Dk.Isdor Mpango amesema Serikali ya Tanzania imefanya kazi na nchi ya Cuba miaka mingi tangu Mwaka 1962.

Amesema imekuwa ikifanya kazi nayo katika sekta ya utalii,elimu,kilimo na afya tangu miaka hiyo hali inayoonyesha ushirikiano huo ulivyo muhimu.

“Tumekubaliana kuongeza ushirikiano baina yetu katika sekta mbalimbali ili kuongeza nguvu katika uimarishaji wa sekta hizo na kuhakikisha ushirikiano unaendelezwa ,”amesema Dk.Mpango.

Amesema Tanzania itaendelea kutumia nguvu kuhakikisha vikwazo vya kiuchumi vinaondolewa katika nchi ya Cuba.

Aidha amesema Serikali ya CUBA inatarajia kuandaa Mkutano mkubwa kwa kukuza Kiswahili kwa Ukanda wa ‘Latin America’ hivyo Tanzania itaunga mkono katika mkutano huo.

Kwa upande wake Makamu wa Rais Cuba, Salvador Valdes Mesa amesema amefurahia mazingira na mapokezi ya Tanzania kwa serikali ya Cuba na uhusiano mkubwa wa nchi hizo mbili tangu mwaka 1962.

Amesema uhusiano huo umeendelea kuimarishwa katika masuala ya afya, elimu, kilimo, utalii na kuongeza sanaa na michezo.

“Katika hati ya makubaliano haya tuliosaini leo ikiwemo masuala ya dawa tumejenga kiwanda cha viuatilifu vya maralia Kibaha ambapo kinatoa dawa za binadamu na kuendelea kuzalisha dawa za mbu zitokanazo na mimea na kuendeleza kiwanda katika mazingira ya kileo na teknolojia,”amesema Mesa.

Amesema kiwanda hicho katika Afrika kipo Tanzania tuu lengo ni kuzalisha dawa na kuboresha aina za dawa ambazo zinazozalishwa.

Mesa amesema nchi ya Cuba bado inaendelea kupambana na kushirikiana na jamii katika maendeleo, hivyo wameendelea katika madawa na teknolojia.

Vilevile amesema kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika siasa na uchimu kwa manufaa ya mataifa hayo.

Aidha amesema Tanzania imekuwa bega kwa bega kuingolea Cuba miaka yote pamoja na kupata vikwazo inaendelea kusimama na haiwezi kupoteza uzalendo wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles