25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Kocha Salum Suleman ashauri wachezaji Taifa Stars

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

KOCHA wa zamani wa timu za Al – hamra, Al nadha za nchini Oman, Salum Suleman Salum amewashauri wachezaji wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ kucheza kwa kujiamini bila hofu katika michezo yake ya kundi F kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) yanayofanyika kuanzia Januari 13, mwaka huu chini Ivory Coast.

Taifa Stars imepangwa kundi FC pamoja na timu za Morocco, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Zambia ambapo itacheza mchezo wake wa kwanza Januari 17 dhidi ya Morocco.

Salum ambaye ana leseni D Diploma ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) alianza kazi ya kufundisha soka katika klabu ya Shangani Zanzibar mwaka 1981 ambayo pia alicheza soka lake mwaka 1974 hadi 1980.

Pia, alifundisha timu za Malindi, shule za sekondari Ben Bella, Haile Selassie, Spars FC, Zanzibar Junior Combine, Kibweni na Sharp Boys zote za Zanzibar, huku nje ya nchi akifundisha soka nchini Oman katika klabu za Yanqul, Ibir, Al Hamra na Al Nahdha.

Akizungumza na Mtanzania Digital kwa simu kutokea nchini Oman yalipo makazi yake, Salum amesema anaamini kocha mkuu wa taifa stars, Adel Amrouche atashangaza watu na kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri katika mashindano hayo licha ya kupangwa na wapinzani wagumu.

“Nimewatazama kwenye mechi mbalimbali mpaka sasa tunacheza vizuri pia ukiangalia kundi tulilopo nawashauri timu yangu ya Taifa Stars kucheza bila ya hofu na wajiamini, lakini mashabiki wawe na uzalendo waweke utaifa kwanza,” alisema Salum ambaye kwa sasa anafundisha All Star Academy ya Zanzibar

Akizungumzia soka la Tanzania, Kocha huyo amesema limepiga hatua ikiwemo Ligi Kuu na yuko tayari kufanya kazi na timu yoyote ambayo itamfuata na kutaka wafanye kazi kwani amekuwa akifanya nao mazungumzo ya masuala mbalimbali ya mchezo wa soka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles