Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital
Taasisi ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC), imekabidhi baiskeli mwendo 12 ‘wheelchairs’ kwa timu ya mpira wa kikapu cha watu wenye za ulemavu ‘wheelchair basketball’.
Baiskeli hizo zinazotumika kuchezea mchezo huo, vimekabidhiwa leo Novemba 23, 2023 mbele Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Neema Msitha amevitaka vyama vya michezo nchini kuwa wabunifu ili kushawishi wadau kushiriki katika jithada za kukuza michezo nchini.
“Niwapongeze Chama Cha Mchezo wa Kikapu cha Watu wenye za ulemavu Tanzania kwa kuendelea kukuza mchezo huu kwa kuhusisha wadau mbalimbali. Nitoe rai kwa vyama vingine vya michezo kuwa wabunifu na kujipambanua ili kuwashawishi wadau,” amesema Neema.
Naye Katibu wa Chama Cha Mchezo wa Kikapu cha Watu wenye za ulemavu Tanzania (TWBA), Abdallah Mpogole, ameishukuru ICRC kutokana na mchango wao wa kuwasadidia vifaa vya mchezo huo mara kwa mara.
“Tunaishukuru ICRC kwa msaada huu ambao sio mara ya kwanza, mara nyingine tuliweza kupeleka, mikoa ya Kilimanjaro, Iringa na Zanzibar, na nia yetu ni kufika mikoa yote ili mchezo huu, uchezwe kila pande ya nchi,” amesema.