Necta yafungia vituo viwili kwa udanganyifu
Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital
Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa Darasa la Saba huku ufaulu ukiongezeka kwa asilimia 80.58 ya watahiniwa 1,356, 296.
Pia, limevifungia vituo viwili ambayo ni Twibhoki na Graiyaki vilivyopo Halmashauri ya Serengeti mkoani Mara kwa kuthibitika kufanya udanganyika katika mtihani huo.
Akizungumza leo Novemba 23, jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Said Mohamed amesema jumla ya watahiniwa 1,397,293 walisajiliwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi, wasichana wakiwa 742,690 sawa na asilimia 53.15 na wavulana 654,603 sawa na asllimoa 46.85 huku wenye mahitaji maalumu wakiwa 4,599 sawa na asilimia 0.33.
“Jumla ya watahiniwa 1,092,960 sawa na asilimia 80.58 ya watahiniwa 1,356,296 wenye mtokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka huu, wamefaulu na kupata madaraja ya A,B na C.
“Wavulama waliofaulu ni 507,920 sawa na asilimia 80.59 na wasichana ni 585,040 sawa na asilimia 80.58 huku mwaka jana watahimiwa waliofaulu walikuwa 1,073,402 sawa na asilimia 79.62 hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.96,”amesema Dk. Mohamed.
Katika ubora wa ufaulu, watahiniwa wengi wamepata daraja la B na C ambapo daraja B ni watahiniwa 314,646 sawa na asilimia 23.20 , daraja C ni watahiniwa 724,371 sawa na asilimia 53.41 na watahiniwa 53,943 sawa na asilimia 3.98 wamepata daraja la A.
Amesema ubora wa ufaulu kwa wasichana umeongezeka na kufikia asilimia 80.58 ikilinganishwa na asilimia 78.91 katika mwaka jana ambapo ongezeko.kwa daraja A ni asiliki 0.13, daraja B ni (0.96),C(0.57).
Pia ubora wa ufaulu wa wavulana nao umeongezeka hadi asilimia 80.59 ikilinganishwa na asilimia 80.41 mwaka jana ambapo ongezeko kwa asaraja A ni asilimia 0.42,B(0.58) na C umeshuka kwa silimia 0.83.
UFAULU WA KIMASOMO
Dk. Mohamed amesema kwa upande wa ufaulu wa kimasomo katika sayansi ya teknolojia ni asilimia 74.08 na somo la hisabati ni asilimia 48.83, ambapo katika somo la sayansi na teknolojia umepanda kwa asilimia 2.45 na somo la hisabati umeshuka kwa asilimia 4.46 ikialinganishwa na mwaka jana.
Amesema katika somo la sayansi na teknolojia wavulana wana ufaulu wa asilimia 75.78 na wasichana wana ufaulu wa asilimia 72.60 na somo la hisabati wavulana wana ufaulu mkubwa wa asilimia 52.45 kuliko wasichana ambao wana ufaulu wa asilimia 45.69.
Kwa upande somo la lugha ya Kingereza ufaulu ni asilimia 34.35 na ufaulu wa somo la kiswahili ni asilimia 87.91 ambapo katika somo la English Language umepanda kwa asilimia 4.96 na somo la kiswahili umeshuka kwa asilimia 1.59 ikilinganishwa na mwaka 2022.
Amesema katika somo hilo wavulana wana ufaulu wa asilimia 34.39 huku wasichana wanakiwana ufaulu wa asilimia 34.32 ambapo somo la kiswahili wasichana wanaufaulu mkubwa wa asilimia 88.91 kuliko wavulana ambao wana ufaulu wa asilimia 86.76.
Vilevile amesema kwa upande wa ubora wa ufaulu katika somo la Kiswahili umeongezeka Kwa watahiniwa waliopata daraja la A hadi asilimia 30.44 ikilinganishwa na asilimia 29.96 katika mwaka 2022 huku japokuwa asilimia ya watahiniwa waliopata daraja B imepungua kwa asilimia 2.01 .
“Katika somo la English Language ubora wa ufaulu umeongezeka Kwa watahiniwa waliopata daraja la A na B hadi ufaulu asilimia 11.40 ikilinganishwa na asilimia 8.65 katika mwaka 2022,”amesema.
Katika masomo ya Sanaa Dk Mohamed aameeleza kuwa ufaulu wa somo la maarifa ya jamii na stadi za kazi ni asilimia 77.40 huku somo la uraia na maadili ni asilimia 82.12 ambapo katika somo la maarifa ya jamii na stadi za kazi umepanda kwa asilimia 6.17 na somo la uraia na maadili umepanda kwa asilimia 0.25 ikilinganishwa na mwaka 2022 .
Aidha katika somo la maarifa ya jamii na stadi za kazi wavulana wana ufaulu wa asilimia 79.41 na wasichana wana ufaulu wa asilimia 75.66 na somo la uraia na maadili wavulana wana ufaulu wa asilimia 81.96 na wasichana wana ufaulu wa asilimia 82.25.
Dk.Mohamed amesema idadi ya shule katika makundi ya umahiri inaonesha kati ya shule zote 18,314 zenye matokeo, shule 13,822 sawa na asilimia 75.47 zimepata wastani wa daraja C ukilinganisha na madaraja mengine ya ufaulu.
Amesema shule zilizopata wastani wa daraja A hadi C zimeongezeka kwa asilimia 1.71 kutoka idadi ya shule 16,294 sawa na asilimia 92.73 mwaka huu na hakuna shule yenye wastani wa daraja E.
MATOKEO YALIYOZUIWA NA KUFUTWA
Pia NECTA imezuia matokeo ya watahiniwa 360 ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani kwa masomo yote au idadi kubwa ya masomo.
Amesema watahiniwa husika wamepewa fursa ya kurudi kufanya mtihani wa kumaliza kumaliza elimu ya msingi kwa mwaka ujao kwa mujibu wa kifungu cha 32 (1) cha kanuni za mitihani.
Vilevile NECTA limefuta matokeo yote ya watahijiwa 31 sawa na asilimia 0.002ya watahiniwa 1,356,392 waliofanya mtihani ambao wamebainika kufanya udanganyifu katika mtihani wa kumaliza elimu hiyo.
SHULE ZILIZOFUNGIWA KUWA VITUO
Dk.Mohamed amesem NECTA imefungia vituo viwili ambayo ni Twibhoki na Graiyaki vilivyopo halmashauri ya Serengeti mkoani Mara kwa kuthibitika kufanya udanganyika katika mtihani huo hadi watakapojiridhisha kuwa ni salama kwa uendeshaji wa mitihani ya taifa.
SHULE ZILIZOPEWA ONYO
Pia Baraza hilo limeziandikia barua za onyo vituo vya mtihani vinne ambavyo ni Mother of Mercy, St.Marys Mbezi Beach vya Halmashauri ya Kinondoni na Charm Modern cha Halmashauri ya Karatu mkoa wa Arusha.
Amesema pamoja na Morotonga cha halmashauri ya Serengeti mkoa wa Mara ambavyo vilijaribu kujihusisha na vitendo vya udanganyifu katika mtihani na vituo hivyo vitakuwa chini ya ungalizi wa baraza hilo hadi hapo NECTA latakapojiridhisha kuwa ni vituo salama kwa uendeshaji wa mitihani ya Taifa.