27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyabishara Mkuranga walia zuio biashara ya mkaa

Na Mwandishi Wetu, Mkuranga

Wafanyabiashara wilayani Mkuranga wameiomba serikali kuruhusu biashara za uuzaji wa mkaa kwasababu wananchi wengi hawamudu gharama za kutumia gesi.

Ombi hilo limetolewa na mfanyabiashara Yasmin Kidawa, wakati akizungumza kwenye mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara (JWT) wilayani humo katika mwendelezo wa ziara ya kusikiliza kero za wafanyabishara mkoani Pwani.

Amesema kwa sasa hawawezi kumudu gharama za kununua gesi, hivyo wakati wa kujipanga kuangalia namna ya kupunguza gharama za gesi wanaomba kuruhusiwa kwa matumizi ya mkaa.

“Tunafahamu nia ya serikali ni nzuri, lakini hali ya maisha ya wananchi wa Mkuranga ni ngumu, bado hatuwezi kumudu gharama za gesi. Tunaomba serikali ituache tuendelee kutumia mkaa badala ya kuzuia bila kuangalia hali yetu kiuchumi,” amesema Kidawa.

Naye mfanyabishara Jumanne Mohamed, amesema wananchi wa wilaya hiyo wanakabiliwa na changamoto kubwa ya umasikini.

Amesema biashara kubwa wilayani humo ni bidhaa za misitu lakini kutokana na kuzuiliwa kwa biashara ya mkaa, wamezidi kuwa masikini kwa sababu wengi hawamudu bei ya mkaa lakini pia gharama ya gesi ni kubwa.

Amesema serikali inatakiwa kupunguza bei ya gesi ili kila Mtanzania amudu kutumia na kupunguza matumizi kuliko kuzuia matumizi ya mkaa kwa kuweka ushuru wa Sh. 6,000 kwa kiroba na gharama kubwa ya gesi. 

Amesema gharama ya mkaa kwa kiroba kidogo ni Sh 12,000 hadi 15,000 wakati awali walinunua kwa Sh 3,000 hadi 4,000.

Aidha, wamewalalamikia maofisa wa Wakala wa Misitu (TFS), kuwanyang’anya wafanyabishara wa mkaa mizigo yao na kuiuza badala ya kuiteketeza.

“Kama mmepiga marufuku uuzaji wa mkaa, mnapowanyang’anya wafanyabishara iteketezwe sio wanaichukua na wao wanaenda kuiuza maana yake ni kutukwamisha sisi lakini siyo kuzuia biashara ya mkaa,” amesema.

Mwenyekiti wa JWT, Hamis Livembe, ameahidi kuifikisha kero hiyo ngazi ya halmashauri ili zifanyiwe kazi na wenye mamlaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles