29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Livembe: Wafanyabiashara tunajivunia Rais Samia

Na Mwandishi Wetu, Kisarawe

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Hamis Livembe, amewataka wafanyabiashara nchini⁷ kufanya kazi kwa bidii kwa sababu Rais Samia Suluhu Hassan ameifungua nchi kiuchumi.

Amesema wana wajibu wa kujivunia juhudi za Rais Samia katika kushughulikia kero zao na kufungua milango ya majadiliano jambo ambalo halikuwahi kufanyika miaka ya nyuma.

Livembe ameyasema hayo leo Novemba 7,2023 wakati akizungumza na wafanyabishara wilayani Kisarawe mkoani Pwani, katika mwendelezo wa ziara za viongozi wa JWT kusikiliza kero za wafanyabiashara nchi nzima.

Amesema awali wafanyabishara walikuwa hawana nafasi ya kusikilizwa isipokuwa inapotokea migomo na maandamano lakini tangu utawala wa Rais Samia, wamepewa nafasi ya kujisemea na kusikilizwa.

“Tutembee kifua mbele, tufanye biashara kwa amani na utulivu, bila kusahau kutimiza wajibu wetu. Tumekutana hapa leo tujadili matatizo yetu kipi kinatukwamisha kufanya biashara kwa utulivu ili kwa kushirikiana na serikali tukae meza moja na tuyamalize,” amesema Livembe.

Ametolea mfano wa moja ya kero ambazo imefanyiwa kazi ni faini ya kutokutoa risiti kwa mteja au kutoandika jina ambayo awali ilikuwa Sh milioni 4.5 lakini imeshushwa hadi Sh milioni 1.5 baada ya wafanyabishara kulalamika.

Naye Mjumbe wa Bodi ya Uongozi ya JWT, Ismail Masoud, amesema katika mikoa 12 waliyopita wamesikiliza kero nyingi ambazo zinafanana na tayari nyingine zimeanza kufanyiwa kazi.

Nao wafanyabiashara wa Wilaya ya Kisarawe, wamelalamikia kodi za kero zinazotozwa na halmashauri na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikiwamo ya jengo la fremu anayotozwa mpangaji badala ya mwenye nyumba.

Ziara hiyo inaendea katika Wilaya za Kibiti na Mkuranga mkoani humo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles