33.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

TASAC yakiri ina changamoto

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

SHIRIKA la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema linakabiliwa na changamoto nyingi zinazotokana na wateja wao kukosa  nyaraka na wengine kuchelewa kuziwasilisha ili kutoa mizigo kwa wakati.

Kutokana na hali hiyo, uongozi wa TASAC na wadau wake leo Oktoba 26,2023 wamekutana jijini Dar es Salaam kwa lengo  la kujadili jinsi ya kutatua changamoto hiyo.

Kaimu Meneja Ugomboaji na Uondoshaji wa Shehena wa TASAC, Michael Polycarp amesema shirika hilo wajibu wake ni kutekeleza majukumu ya wadau mbalimbali pamoja na kuboresha huduma kwa wateja.

Ametaja shughuli wanazofanya ni ugomboaji wa bidhaa tano pekee ambazo ni silaha, nyaraka za serikali, wanyamapori, kemikali na makinikia.

Wadau wa TASAC

Polycarp amesema kabla ya sheria kubadilishwa walikuwa na bidhaa 15 za ugomboaji sasa wamebaki na tano huku asilimia 96 ya wateja kupungua kutokana na mabadiliko ya sheria ikiwa tofauti na miaka ya nyuma.

“Kuna changamoto nyingi kutoka kwa wateja ikiwemo kutokuleta nyaraka kwa wakati, nyaraka hazifanani, kuchelewa kulipa kodi na muda mwingine kodi inalipwa lakini katika mfumo wa taasisi za fedha inaoneka bado haijalipwa,”amesema Polycarp.

Amesema TASAC kwa kukutana na wadau wa taasisi za serikali na sekta binafsi, watashirikiana kutatua changamoto zinazowakabili na kutoa mapendekezo na nini kifanyike.

Naye Mwakilishi wa Kampuni ya Oxley Limited, John Akuti amesema wamekutana  kujadili changamoto ya ucheleweshaji wa kutoa mzigo Bandarini  anaamini watapata mfumo rafiki kati ya mteja na TASAC.

Kwa upande  wake Mwakilishi wa Kampuni Seefooth General Agencies Limited,  Neema Mollel  amesema  wamekutana na TASAC wachukue maoni yao  ili wayafanyiwe kazi.

“Changamoto kuna baadhi ya sheria zinawekwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na miongozo zinatofautiana na TASAC zinakuwa changamoto kwa wateja,”amesema Neema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles