Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeahidi itaendelea kuwafikia wateja wake kwenye maeneo mbalimbali ili kuhakikisha wanawasaidi kusajili kampuni na kutatua changamoto zao zinazowakabili.
Akizungumza leo Oktoba 8, jijini Dar es Salaam Afisa Leseni BRELA, Koyan Aboubakar kwenye onesho la saba la Site swahili Internation tourism Expo amesema katika onesho hayo wamefanikiwa kusajili wateja wapya zaidi ya 50.
“Ushiriki wetu kwenye maonyesho haya ya utalii ili kuwasaidia hawa wenye makampuni ya utalii amabao hawajasajili au kuhuisha taarifa zao pamoja na kutoa elimu ya umuhimu wa kusajili kampuni zao,” amesema Aboubakar.
Amesema biashara ya utalii imekua sana nchini hivyo wanaojihusisha na biashara hiyo ni vyema kujisajili ili kuwa na leseni zao za biashara.
Amesema tangu kuanza onesho hilo oktoba 6 hadi leo Oktoba 8, wameweza kutatua changamoto mbalimbali za wateja.
“Changamoto kubwa tunayokutana ni elimu ya jinsi ya kutumia mtandao kwenye kujisajili na kuhuisha taarifa zao hapa kwa muda wa siku hizi tatu tumeshasaidia watu zaidi ya 50,” amesema.
Aidh, amesema wataendelea kutoa elimu kuhusu majukumu ya BRELA kwa wananchi na wadau mbalimbali.