22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Biteko awataka Ma-RC, DC kuwa wabunifu

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amewasisitiza Wakuu wa mikoa na wilaya kuwa wabunifu kutangaza fursa za utaliii na kuwahimiza Watendaji kutimiza wajibu wao wa kuwahudumia Watanzania.

Dk. Biteko ameyasema hayo Oktoba 7, jijini Dar es Salaam wakati akizindua mpango mkakati wa kutangaza fursa zilizopo katika sekta ya utalii katika Wilaya ya Pangani katika Kongamano la Uwekezaji la Swahili International Tourism Expo lenye lengo la kutangaza fursa za uwekezaji zilizoko katika wilaya hiyo ikiwemo utalii katika mbuga ya Saadani, fukwe, kilimo biashara pamoja na uchumi wa buluu.

Amesema kongamano hilo litumike kuitangaza wilaya ya Pangani na kubadilishana mawasiliano ili fursa zilizoko wilayani humo ambazo hazipatikani kwengine zishawishi watu wengine kuzifuata.

“Niwapongeze sana watu wa Pangani kupitia Mkuu wa Wilaya kwa ubunifu huu wa hali ya juu na nitoe wito kwa wilaya zingine kuiga Pangani na kufungua fursa za utalii na uwekezaji kwenye wilaya zao,” amesema Dk. Biteko.

Amesema fursa zilizopo Sekta ya Utalii katika wilaya ya Pangani, mkoani Tanga ni kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuikuza sekta hiyo nchini.

Upande wake, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Dunstan Kitandula amesema kuwa, sekta ya utalii kwa sasa mchango wake katika Pato la Taifa ni asilimia 17.

Amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira rafiki katika sekta hiyo ili kuendelea kuvutia utalii nchini katika maeneo mbalimbali hususan wilaya ya Pangani.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Zainabu Abdallah amesema, wilaya hiyo imejikita kwenye uwekezaji wa maeneo matatu ikihusisha utalii, kilimo mkakati na uchumi wa buluu na kuongeza kuwa wilaya hiyo ni miongoni mwa wilaya ya kimkakati yenye mazingira mazuri ya uwekezaji.

“Serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji na tunawaomba wawekezaji kufika wilaya ya pangani kujionea fursa hizo muhimu,” alisisitiza Zainabu

Uzinduzi wa mpango huo ulikwenda sambamba na kongamano la uwekezaji chini ya maonyesho ya wadau wa Sekta ya Utalii kuunga mkono fursa za uwekezaji waliohudhuria hafla hiyo ni Viongozi mbalimbali wa Serikali, watendaji wa taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo na wadau wa sekta ndani na nje ya nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles