29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na GGML

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ameahidi Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwamba Serikali itaendelea kuwaunga mkono ili kuifanya sekta ya madini kukua na kuwafanya Watanzania wafaidike na rasilimali ambayo Mungu amewajalia.

Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong akihutubia washiriki wa maonesho ya sita ya teknolojia ya madini Geita yanayoendelea katika viwanja vya Bombambili-EPZ mjini Geita. 

Pia ametoa wito kwa uongozi wa kampuni hiyo kumpa ushirikiano wa kutosha Waziri mpya wa madini, Anthony Mavunde ili atimize malengo aliyojiwekea hasa ikizingatiwa GGML ndio mgodi mkubwa wa madini ya dhahabu kuliko migodi yote iliyopo nchini.

Dk. Biteko ametoa kauli hiyo Septemba 23, 2023 alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya sita ya teknolojia ya madini Geita pia katika hotuba yake ya kufungua maonesho hayo yanayoendelea katika viwanja vya Bombambili-EPZA Geita mjini.

Awali akizungumza katika banda la GGML, Dk. Biteko amesema kampuni hiyo imekuwa mshirika mkubwa wa serikali lakini pia anafarijika kwa kuwa mwekezaji hai kupitia mpango wa uwajibikaji kwa jamii.“Hata mkuu wa mkoa wa Geita (Martin Shigela) amesema ninyi ndio wadhamini wakuu wa maonesho haya kwa hiyo tunawapongeza sana,” amesema.

Amesema kwa kuwa sasa sekta hiyo inaye waziri mpya, yeye inawezekana alikuwa waziri mpole kidogo lakini sasa amekuja waziri Mavunde ambaye ni mkali hivyo apewe ushirikiano.

“Mpeni ushirikiano ili sekta hii tuitoe izidi kukua kwa sababu mgodi wa GGML ndio mfano wa migodi yote nchini kwa hiyo tusipofanya vizuri Geita na migodi mingine haitafanya vizurim tukifanya viziru migodi mingine itafanya vizuri. Lakini nawapongeza sana,” amesema Dk. Biteko.

Aidha, akizungumza katika ufunguzi wa maonesho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuboresha mazingira rafiki kwa wawekezaji nchini.Strong amesema jitihada Rais Samia kufuatilia kwa umakini sekta binafsi na sekta ya madini na kutatua changamoto zke, zimeibua matumaini katika eneo wadau wengi wa sekta hizo nchini.

“GGML inaweza kuwa mfano wa kuigwa kutokana na ari hii mpya, baada ya kupata ushirikiano wa kutosha kutoka Serikalini mathalani katika utekelezaji wa sheria mpya ya madini,” amesema.

Amesema sheria hiyo imetoa mwongozi wa usimamizi wa sekta ya madini kuhusu masuala ya kodi, malipo ya mrabaha, na matumizi ya fedha za uwajibikaji wa kampuni kwa jamii, huku pia ikisisitiza ujumuishaji wa uchumi wa ndani.

“Tunafarijika kusema kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, GGML imeshirikiana kwa kiasi kikubwa na Serikali ya mkoa wa Geita, kwa kutenga zaidi ya Sh bilioni 46 kupitia Mfuko wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR). Fedha hizi zimesaidia kutekeleza miradi kadhaa inayolenga jamii ikiwemo ujenzi wa soko la kisasa na vituo vya huduma ya afya ikiwemo miundombinu ya elimu inayolenga mahitaji ya ndani,” amesema.

Pia amesema maonesho hayo ambayo mwaka huu GGML ni mdhamini mkuu, kampuni hiyo inajihisi faraja kuona yanapiga hatua na kuwa kitovu kkuu cha biashara na uwekezaji hasa baada ya GGML kutumia uboreshaji wa eneo hilo la Mamlaka ya Maeneo ya Uzalishaji Bidhaa kwa Mauzo ya Nje (EPZA) yenye ukubwa wa ekari 200.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles