29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yajipanga kuendeleza ubabe Cana Zone III

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Chama Cha Kuogelea Tanzania(TSA), kimesema kimejipanga kutetea ubingwa wao katika mashindano ya Kanda ya ‘Cana Zone III’, yatakayofanyika Novemba 23-26, 2023, Kigali nchini Rwanda. Kauli hiyo imetolewa na Rais wa TSA, David Mwasyoge wakati wa kufunga mashindano ya Taifa ya Kuogelea Septemba 24,2023, Masaki, Dar es Salaam.

Mwasyoge amesema kuelekea mashindano hayo, Kamati ya Ufundi itakutana kuchagua wachezaji 30 ambao wana viwango vinavyohitajika na kuweka kambi jijini kabla ya kwenda Rwanda.

“Kumbuka sisi tunakwenda Rwanda tukiwa mabingwa watetezi, lengo letu mwaka huu ni kuhakikisha tunatetea ushindi wetu, hivyo kamati itakaa na kuchagua wachezaji waliofikisha viwango vinavyotakiwa kwenye mashindano ya Kanda.

“Tunaomba Serikali na wadau wengine watusapoti ili vijana wengi wapate nafasi kwa sababu kupeleka vijana 30 Rwanda sio kazi ndogo kwa kuwa kuna gharama za nauli, maladhi na vitu vingine,” amefafanua Mwasyoge.

Kwa upande wake mwakilishi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Charles Mazugu ameipongeza TSA na kuahidi kuwa pamoja nao kwa kuwa kama Serikali ni jukumu lao kuziangalia timu za Taifa.

Mazugu amesema katika mashindano ya Taifa ameshuhudia ushindani mkubwa klabu zilizoshiriki, huku akifurahishwa na uwepo wa vijana wadogo wenye vipaji vikubwa vya kuogelea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles