25.1 C
Dar es Salaam
Monday, October 28, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mollel: Msongo wa mawazo kwa mjamzito unaathiri afya ya mtoto

Na Patricia Kimelemeta, Mtanzania Digital

NAIBU Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel amesema kuwa msongo wa mawazo kwa mjamzito ni miongoni mwa sababu zinazoathiri afya ya Mtoto akiwa tumboni.

Akizungunzia mkoani Dar es Salaam katika uzinduzi wa wiki ya unyonyeshaji inayoadhimishwa kila mwaka kuanzia tarehe 1 hadi 8, ambapo Dk. Mollel amesema kuwa wajawazito wanatakiwa kukaa katika mazingira yasiyowaletea msongo wa mawazo katika kipindi chote cha ujauzito na hata wanapojifungua na kuyonyesha ili kufanya maziwa yatoke vizuri na mtoto kupata lishe bora na kukua vizuri.

Amesema kuwa mjamzito anahitaji matunzo na kula vyakula vyenye virutubisho kwa. ajili ya lishe bora ya mtoto tangu kutungwa kwa mimba hadi mtoto anapofikisha umri wa miaka miwili Kwa sababu ndiyo kwenye msingi bora wa ukuaji wa mtoto kimwili na kiakili.

Dk. Mollel alisema, kuwa idadi ya watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee imeongezeka kutoka 58% mwaka 2018 hadi kufikia 64% mwaka 2022.

“Takwimu ya watoto wanaonyonyeshwa ndani ya saa 1 baada ya kuzaliwa imeongezeka kutoka 53.5% mwaka 2018 hadi kufikia 70% mwaka 2022.

“Siku 1000 za mwanzo, mtoto anahitaji lishe bora ambayo itajenga afya ya mtoto ili aweze kukua kimwili na kiakili, hii inatokana na mama anayenyonyesha kupata lishe bora ambayo itajenga kiafya na kumuondolea msongo wa mawazo,” amesema Dk. Mollel.

Ameongeza kuwa, hayo ni mafanikio makubwa ambapo Serikali itaendelea kuahirikiana na wadau mbalimbali Ili kutoa elimu kwa wananchi kuona umuhimu wa kumnyonyesha watoto.

Amesema kuwa ikiwa hatakosa lishe bora linaweza kumsababishia msongo wa mawazo ambapo mtoto hatakosa lishe bora na kumsababishia kupata madhara mbalimbali ikiwamo udumavu wa mwili na akili.

Amesema kuwa, hivyo ni muhimu mtoto kunyonyeshwa maziwa ya mama pekee kwa muda wa miezi sita ya mwanzo na hapo anaweza kuendelea kunyonyeshwa huku akipatiwa chakula cha nyongeza hadi anapotimiza miaka miwili au zaidi.

Amesema kuwa watoto wadogo na watu wazima wanapaswa kula lishe bora ili kuimalisha afya zao na kuwaepusha na magonjwa yanayotokana na kutokula lishe isiyokamilika.

“Kuna magonjwa mengi yanayotokana na kutokula lishe kamili ni vyema watoto na watu wazima kuzingatia hilo, pia lishe inayozidi inasababisha uzito uliozidi na hivyo kusababisha magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Figo na moyo,” amesema.

Naye, Mwakilishi wa wadau wa Lishe nchini kutoka UNICEF, Patrick Codjia ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa dhamira ya dhati ya kuboresha lishe, afya na maisha ya wananchi wake ikiwa ni pamoja na watoto.

“UNICEF itaendelea kuahirikiana na serikali ya Tanzania ili kuboresha afya ya watoto ili waweze kupata lishe bora na kuwaondoa kwenye madhara ya udumavu,” amesema Codjia.

Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO), Chiku Semfuko ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kutoa muda kwa wanawake kwenda kunyonyesha pia kutenga vyumba maalumu vya kunyonyesha ili kuwapa nafasi wanaonyonyesha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles