29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama nchini kuwapiga msasa watumishi wake

Na Mwandishi wetu, Mtanzania Digital

Mahakama ya Tanzania kupitia Kitengo cha Maboresho (JDU) imeandaa Mafunzo ya kujenga uelewa kwa Watumishi wake kuhusu matumizi ya Mfumo mpya wa Serikali wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Mtandao unaojulikana kama (NeST).

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama Agosti 15, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kituo Jumuishi cha Mahakama cha Masuala ya Mirathi na Ndoa Temeke-Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi, Mahakama ya Tanzania, Charles Challe amesema Mafunzo hayo yatasaidia kutekeleza na kusimamia michakato ya ununuzi ya Taasisi, kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na kuleta uwazi.

“Ninawaomba washiriki kufuatilia mafunzo haya kwa kina kwa manufaa ya Mahakama, Wazabuni, Wananchi na Taifa kwa ujumla hatimaye Watanzania kupata thamani ya fedha zao za kodi na vilevile kuondokana na hoja za ukaguzi zisizo na msingi,” amesema Challe.

Amesema kuwa, Mafunzo hayo ya siku tano yanatolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Mamlaka ambayo ndiyo iliyobuni Mfumo huo na ndio wenye jukumu la kutoa mafunzo na kusimamia utekelezaji wake.

“Mnatakiwa kuwa na umakini mkubwa sana kwani uelewa na utekelezaji wa mfumo huu ni matakwa ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ili kuwa na matumizi mazuri na sahihi ya fedha za umma katika ununuzi wa vifaa na huduma na hatimaye kuwaletea Watanzania maendeleo yaliyokusudiwa,” amesisitiza Challe.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, Mahakama itaanza matumizi rasmi Mfumo wa ‘NeST’ Oktoba Mosi mwaka huu.

Mafunzo hayo yamehusisha jumla ya washiriki 51 kutoka Idara na Vitengo mbalimbali vya Mahakama. Na katika mafunzo hayo washiriki watapitishwa katika maeneo mbalimbali ya Mfumo ili waweze kuwa na uelewa wa kutosha kabla ya kuanza matumizi rasmi

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles