25.7 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi kata ya Misugusugu wawapa mitano tena Rais Samia, Koka

Na Gustafu Haule,Mtanzania Digital

WANANCHI wa Mtaa wa Zogowale, Saeni na Jonuga iliyopo Kata ya Misugusugu katika Halmashauri ya Kibaha Mjini wamempigia debe Rais wa awamu ya Sita, Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja na mbunge wa Kibaha Mjini, Silvestry Koka kwakusema wanastahili miaka mingine mitano tena baada ya kujengewa zahanati ya kisasa.

Zahanati hiyo imezinduliwa Agosti 11, mwaka huu na mbunge wa Kibaha Mjini, Silvestry Koka ambapo mpaka kukamilika kwake imetumia zaidi ya Sh milioni 181 fedha ambazo zimetoka Serikali Kuu, mfuko wa jimbo na mapato ya ndani ya Halmashauri .

Wakizungumza katika ufunguzi wa zahanati hiyo baadhi ya wakazi wa mitaa hiyo akiwemo Sophia Tebe, amesema awali walikuwa wanasafiri zaidi ya kilomita 30 kufuata huduma ya afya katika Mji wa Mlandizi na katika hospitali ya Tumbi.

Amesema changamoto waliyokuwa wanaipata ni katika usafiri kwani mgonjwa anapotaka kusafirishwa gharama ya usafiri inakuwa zaidi ya 50,000 huku akisema wajawazito wakati mwingine walikuwa wakijifungulia njiani.

Aidha, Tebe amesema mafanikio ya hupatikanaji wa zahanati hiyo imetokana na juhudi za Serikali ya awamu ya Sita chini Rais Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja Mbunge Koka ambaye amekuwa msimamizi mkubwa katika ujenzi huo.

“Sisi wananchi wa mitaa ya Zogowale, Jonuga na Saeni tunawashukuru sana viongozi wetu hususan Rais Dk. Samia pamoja na mbunge wetu Koka maana wamepambana mpaka tumepata zahanati hii, hakika wanastahili pongezi,” amesema Tebe.

Naye, Halphan Said amesema kuwa hupatikanaji wa zahanati hiyo imekuwa mkombozi kwao kwani walikuwa wanashindwa kufuata huduma za afya katika maeneo mengine kutokana na ukosefu wa fedha.

Said amesema ametambua kuwa viongozi waliokuwa madarakani ni wasikivu kwani walipokwenda kuomba kura waliahidi kutatua changamoto ya zahanati, barabara na maji lakini mpaka sasa vyote vimetekelezeka.

Diwani wa Kata ya Misugusugu, Upendo Ngonyani(CCM) amesema kuwa Zahanati hiyo imeokoa maisha ya wananchi 14,326 wa Kata hiyo waliokuwa wakifuata huduma za afya katika hospitali zilizokuwa mbali nao.

Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa zahanati hiyo Koka amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita ni sikivu na kwamba wananchi watembee kifua mbele kwakuwa imejipanga kutatua changamoto za wananchi wake.

“Nilikuja hapa kipindi cha kampeni nikawaahidi zahanati na nilianza kwa kutoa milioni tano na baadae nikatoa milioni moja na nusu na ndipo serikali ikatubeba na leo tunafungua zahanati yetu,kwahiyo niwaombe tuendelee kushirikiana kwa ajili ya kutatua kero nyingine,” amesema Koka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini, Mwajuma Nyamka, amesema kuwa kazi ya CCM ni kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma zote za kijamii hivyo waendelee kukiamini chama kwakuwa kinaweza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles