Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Wizara ya Madini imeendelea kupokea Maoni ya Wadau wa sekta hiyo kuhusu mapendekezo ya Marekebisho ya Sheria na baadhi ya Kanuni zitakazosimamia shughuli za Sekta ya Madini nchini.
Akiongoza Kikao Kazi leo Agosti 2, jijini Dar es Akinachoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Dk. Suleiman Serera amewataka wadau wa sekta ya madini kuchangia mawazo yao kwa uhuru ili kuboresha na kuongeza ufanisi katika shughuli za sekta hiyo.
“Ametaja maeneo yatakayopokelewa mapendekezo yake na kujadiliwa kuwa ni Kanuni ya Madini Ushiriki wa Serikali za Mwaka 2022, Kanuni ya Eneo Tengefu la Mirerani za Mwaka 2022, Kanuni ya Haki Madini za Mwaka 2018, Kanuni ya Masoko ya Madini za Mwaka 2019 pamoja na Kanuni za Uongezaji Thamani Madini za Mwaka 2020,” amesema Dk. Serera.
Naye Kamishna Msaidizi upande wa Mazingira, Mhandisi Ally Samaje amezitolea ufafanuzi Kanuni mbalimbali zinazopendekezwa ambapo amesema kuna baadhi ya Kanuni zina changamoto katika utekelezaji wake ambapo suluhisho lake ni kuzifanyia Marekebisho.