22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaokoa Bilioni 192 matibabu nje ya nchi

N Mwandishi Wetu, Dodoma

SERIKALI imeokoa Sh bilioni 195.2 ambazo zingetumika nje ya Nchi kwa ajili ya matibabu.

Hayo yameelezwa leo, Alhamisi Agosti 3,2023 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Profesa Abel Makubi wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya Taasisi hiyo ndani ya miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita na mipango ya mwaka 2023-2024 kwa Waandishi wa Habari.

Prof. Makubi amesema kama wagonjwa hao wangepelekwa nje ya nchi kwa matibabu jumla ya Sh bilioni 231.6 zingetumika.

Mkurugenzi huyo wa MOI amesema Serikali imeokoa Sh bilioni 195.2 ambazo zingetumika nje ya Nchi kwa ajili ya matibabu

Amesema gharama za matibabu ndani ya nchi zilikuwa Sh za bilioni 36.4.

Prof. Makubi amesema fedha hizo zitatumika kwa shughuli nyingine za maendeleo ya nchi na kupunguza rufaa.

Amesema jumla ya wagonjwa 14,574 walifanyiwa upasuaji ikilinganishwa na wagonjwa 13,618 waliofanyiwa katika 2019/2020 mpaka 2020/2021 ikiwa ni ongezeko la asilimia 3.4%.

Amesema maboresho makubwa ni katika upasuaji wa maeneo ambayo yameendelezwa na kuimarishwa

Pia,Kubadilisha nyonga (Total Hip Replacement) 363,Kubadilisha magoti (Total Knee Replacement) 320

“Upasuaji mkubwa wa mfupa wa kiuno (Pelvic/acetabular surgery) 192 Wagonjwa 481 wamefanyiwa upasuaji wa magoti na mabega kwa njia ya matundu (Knee and Shoulder athroscopic surgery) kati yao waliofanyiwa mabega ni 32 na magoti ni 449,”amesema Prof. Makubi.

Amesema wagonjwa 626 wamefanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo kwa kufungua eneo dogo (minimally invasive spine surgery).

Aidha watoto 41 wamefanyiwa upasuaji wa kunyoosha vibiongo (scoliosis surgery).

Amesema wagonjwa 21 wamefanyiwa upasuaji wa kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo (Aneurysm clipping).

Pia, wagonjwa 423 wamefanyiwa upasuaji kuondoa vivimbe kwenye ubongo kwa njia ya kufungua fuvu (Brain tumour excision surgery).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles