24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 23, 2024

Contact us: [email protected]

TASAC kuboresha udhibiti wa huduma za usafiri wa maji nchini

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetaja mikakati nane ya utekelezaji kwa mwaka 2023-2024 ikiwemo kuboresha udhibiti wa huduma za usafiri na usafirishaji kwa njia ya maji nchini.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Julai 27,2023 na Mkurugenzi wa TASAC, Kaimu Mkeyenge wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Shirika hilo kwa mwaka 2023-2024.

Mkeyenge ameitaja mikakati hiyo ni kuimarisha usalama na ulinzi kwa usafiri kwa njia ya maji sambamba na Udhibiti wa Uchafuzi wa Mazingira utokanao na usafiri wa Meli.

Pia, kuboresha udhibiti wa huduma za usafiri na usafirishaji kwa njia ya maji nchini sambamba na kuweka ushindani ili kuhakikisha huduma za usafiri majini zinakuwa endelevu.

“Kuimarisha Usalama na Ulinzi kwa usafiri kwa njia ya maji sambamba na Udhibiti wa Uchafuzi wa Mazingira utokanao na usafiri wa meli kuboresha usimamizi na uwajibikaji katika kupanga na kutumia rasilimali za Shirika,”amesema Mkeyenge.

Mikakati mingine ni kuimarisha uhusiano ya kitaasisi na kuongeza uelewa wa wadau kuhusu majukumu ya Shirika, kuboresha sheria, kanuni na nyenzo za kiudhibiti katika sekta za usafiri majini na biashara ya meli.

“Kuratibu maandalizi ya Amri, kutoa maoni na kuwezesha uandaaji rasimu za Kanuni na nyenzo za utendaji zitoazo mwongozo kuhusu udhibiti huduma za usafiri majini, usalama na ulinzi kwa vyombo vya usafiri majini na uchafuzi baharini kutoka katika meli,”amesema Mkurugenzi huyo.

Vilevile, kusimamia utekelezaji wa mikataba ya kimataifa kuhusu usafirishaji kwa njia ya maji inayoratibiwa na Shirika la Bahari Duniani (International Maritime Organization).

“Kushirikisha wadau katika kufanya mapitio na marekebisho ya Sheria na Kanuni mbalimbali, ikiwemo Sheria ya Wakala wa Meli Tanzania, sura 415,”amesema Mkeyenge.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.

Naye, Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Serikali inataka kushirikiana na sekta binafsi kuendesha Bandari, mikataba na watakaoendesha bado haijasainiwa.

“Sasa hivi ndio wataalamu wako mezani kuzungumza kuhusu mikataba, muda na gharama.Lakini hakuna Bandari iliyouzwa, wataalamu watakapokamilisha majadiliano tutaangalia maslahi yetu yako wapi na maoni yanayotolewa na Watanzania yatazingatia,”amesema Msigwa.

Amesema Serikali iko macho wakati wote kuhakikisha maslahi ya watanzania yanalindwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles