25.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wazazi Bonyokwa waandikisha wanachama wapya 1,200

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Bonyokwa imefanikiwa kupata wanachama wapya 1,227 katika kipindi cha Januari hadi Juni 2023.

Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Bonyokwa, Mwanairiki Yakub, akizungumza wakati wa kikao cha baraza la jumuiya hiyo.

Kati ya wanachama hao wanawake ni 680 na wanaume ni 547.

Akisoma taarifa ya mpango kazi wa Januari hadi Juni mwaka huu wakati wa kikao cha baraza la jumuiya hiyo, Katibu wa Emau, Jamila Yassin, amesema awali walikuwa na wanachama 961 na sasa wameongezeka na kufikia 2,188.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Wazazi Bonyokwa, Mwanairiki Yakub, amesema wana matawi manne na kwamba wamejipanga kufikia Desemba mwaka huu kila tawi liongeze wanachama 100.

Katika kipindi hicho jumuiya hiyo pia imefanikiwa kuwaunganisha vijana 24 waliomaliza darasa la saba katika mafunzo ya ufundi stadi.

Aidha imemwezesha mtoto aliyekuwa amekaa nyumbani mwaka mmoja bila kwenda shule baada ya mzazi wake kushindwa kumlipia ada katika shule binafsi aliyokuwa akisoma.

Kwa upande wake Mjumbe wa Mkutano Mkuu Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kikao hicho, Tambwe Rashid, amewataka viongozi wa jumuiya hiyo kufanya kazi kwa kushirikiana na kueleza yale yote yaliyofanywa na Serikali ili wananchi waweze kuyajua.

“Jumuiya ya wazazi ndiyo inekibeba chama na moja ya jukumu kuu ni kukiimarisha chama, hivyo viongozi tufanye kazi ya kukisemea chama hasa wakati huu tunapoelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Mama (Rais Samia) anafanya kazi kubwa, tumuunge mkono, tutoke tukawaambie wananchi Serikali ya CCM inafanya nini,” amesema Rashid.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles