24 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania wahimizwa kutumia Kondomu ili kudhibiti VVU

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu wamewataka Watanzania kutumia Kondomu pindi wanaposhiriki ngono ili kujikinga na maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI na kuepuka kupoteza nguvu kazi ya Taifa kutokana na UKIMWI.

Babu ameyasema hayo Mei 10, mkoani Kilimanjaro alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara ya Mkoa huo wakati akitambulisha Kampeini ya Kili Challenge kwa mwaka 2023 yenye lengo la kuchangia jitihada za mwitikio wa UKIMWI nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dk. Leonard Maboko akizungumza na wafanyabiashara wa Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na wadau lengo la TACAIDS kushirikiana na sekta binafsi katika kutafuta raslimali za Mwitikio wa UKIMWI kuwa ni kutokana na kuimarisha vyanzo vya ndani kwa ajili upatikanaji wa fedha za UKIMWI,wanaomsikiliza mbele yake ni meza kuu.

Amesema maambukizi ya VVU na UKIMWI bado ni tatizo nchini ambapo tawimu zinaonesha uwepo wa ongezeko la Maambukizi mapya ya VVU hususan kwenye makundi maalum pamoja na kundi la vijana.

“Jamii inajisahau sana na kufanya mchezo kwa madai ya kwamba ni ajali kazini, kuna kudai kuwa UKIMWI umeisha, hili jambo sio zuri kwani tunakuwa tunajitakia wenyewe, ni vizuri wote tukafahamu na kujua kuwa UKIMWI bado upo kwa mujibu wa takwimu alizotoa Mkurugenzi wa TACAIDS na niwajibu wa kila mmoja kujikinga,” amesema Nurdin.

Amesema kwa hali halisi maambukizi ya VVU bado ya yapo nchini na Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaendelea kupanga na kutekeleza afua mbalimbali za kitabibu na zisizoza kitabibu kwenye mwitikio wa UKIMWI,ambapo kumekuwa na mafanikio makubwa ya kupungua kwa ushamiri wa VVU nchini.

“Pamoja na mafanikio haya yaliyowezeshwa na wadau kutoka nchi mbalimbali na taasisi za kimataifa, kwa sasa ufadhili kutoka nje umepungua hivyo kama nchi hatuna budi kubuni mikakati ya kutafuta raslimali za ndani kwa ajili ya mwitikio wa VVU na UKIMWI ili kupunguza au kuondoa utegemezi wa vyanzo vya nje na kuwa na vyanzo vyetu vya ndani,” amesema Babu.

Aidha, ameipongeza Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGM) kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiutoa kwa serikali hasa katika Mwitikio wa UKIMWI, pamoja na kuchangia fedha kwenye mwitikio wa UKIMWI lakini hutumia nafasi hiyo kuutangaza Mlima Kilimanjaro kitaifa na kimataifa kupitia Kampein ya Kil challenge ambapo watu kutoka nchini,na Mataifa mengine huchangia fedha kwenye mfuko wa kil Trust na kupanda Mlima Kilimanjaro kila mwaka kupitia Kampeini hii ya Kili challenge.

Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko amesema Kili Challenge imekuwa ikifanyika kwa ushirikiano wa TACAIDS na GGM ikiwa ni moja ya hatua za Serikali kushirikisha Sekta Binafsi katika kudhibiti maambukizi ya VVU huku akisisitiza kuwa mapambano bado hayajaisha.

“Mapambano ya VVU bado hatujafikia mwisho, malengo ya kidunia ni kuwa ifikapo 2030 tuwe tumefikia Sifuri tatu kwa maana kuwa tuwe tumemaliza maambukizi mapya, tuwe tumemaliza unyanyapaa na ubaguzi kwa watu wanaoishi na VVU na familia zao  na tuwe tumemeliza vifo vitokanavyo na UKIMWI.

“Kwa upande huo inatia moyo kutokana  na kuwa miaka kumi iliyopita ,mwaka 2010 maambukizi mapya yalikuwa 110,000 kwa mwaka. Kwa takwimu za mwaka 2021 maambukizi mapya ni 54,000 hizi ni takwimu kwa mujibu wa makadirio ya mwaka 2021. Taarifa ya utaifiti mpya wa mwaka 2022/23 umeishaanza na upo katika hatua za mwisho utatolewa ndani ya miezi miwili hadi mitatu ijayo,” amesema Dk. Maboko.

Aidha, Dk. Maboko ameongeza kuwa katika lengo la kumaliza vifo mwaka 2010 kulikuwa na vifo vinavyotokana na UKIMWI watu 35,000, lakini kwa makadirio ya mwaka 2021 ni watu 29,000 na kwamba katika maeneo hayo mawili kama nchi imeshapunguza kwa asilimia 50.

“Kwa upande wa unyanyapaa kwa takwimu za mwaka 2013 zilikuwa ni asilimia 28 na kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2021 unyanyapaa umefika asilimia 5.5. Kwa takwimu hizi bado lengo bado halijafikiwa kwa kuwa lengo ni miaka saba ijayo malengo yote yawe yamefikia sifuri.

“Kwa maana hiyo kwa kadri wafadhili wanavypunguza fedha tunatakiwa kuweka mkazo sana Watanzania wenyewe, kampuni zetu pamoja na wafanyabiashara ndani ya nchi yetu wote tuchangie katika mapambano dhidi ya VVU. Nawahamasisha waalikwa wote tuitikie na kupokea kuwa suala la UKIMWI ni la kila mmoja wetu kwani hakuna Mtanzaia ambaye hajawahi kupata athari za UKIMWI katika maisha yake.

“Pia ni muhimu kulida nguvu kazi katika maeneo yetu ya kazi ili tuweze kutoa maambukizi mapya kwenye 54,000 hadi maambukizi sifuri bado ni kazi kubwa ya kufanya,” alisema Dk. Maboko.

Kuhusu kumalizika kwa vifo vitokanavyo na UKIMWI alisema bado kuna kusuasua sana kwenye kupima ambapo kwa mujibu wa takwimu ni takribani watu 1,700,000 wanakadiriwa kuishi na VVU nchini na waliopo kwenye dawa ni watu 1,500,000 tu.

“Kwa hiyo watu200,000 siyo kazi rahisi, hivyo ushirikiano wa pamoja kwa Watanzania unahitajika ili tufikie malengo ya kidunia ya kumaliza UKIMWI ifikapo 2030.

Naye Makamu wa Rais wa Anglo Gold Ashanti, Simon Shayo aliwaomba waalikwa kutoa ushirikiano wa kuchangia Mwitikio wa UKIMWI kwa kuwa pesa inayopatikana inaenda moja kwa moja kwa wahitaji kupitia TACAIDS baada ya wahitaji kuwasilisha maandiko ya shughuli wanazozitekeleza.

“Kwa ujumla bado kuna makundi mengi ambayo yapo hatarini na yanahitaji kufikiwa na afua mbalimbali za UKIMWI, na kwa bahati mbaya makundi hayo ni yale ambayo ndio nguvu kazi ya Taifa,” amesema.

Ameyataja makundi hayo kuwa ni pamoja na makundi ya vijana, wachimbaji wadogo, wavuvi na madereva wa masafa marefu.

Shayo amewaomba ushirikiano wafanyabiara wa Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na nchi nzima kuwa na ushirikiano kupaza sauti kwa pamoja kwa ajili ya kupambana na VVU lakini pia kutoa raslimali zetu kuchangia chochote ambacho kinaingia kwenye mfuko ambacho mwisho wa siku kinaenda kwa wanufaika ambao unafuata utaratibu maalum wa kuandika andiko ambalo linapitiwa na timu ya pamoja ya GGM na TACAIDS na wadau wengine,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles