29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wajawazito Bukoba waipongeza Serikali

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Baadhi ya akina mama wajawazito wanaopata huduma katika kituo cha afya Zamuzamu kilichopo katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wameipongeza Serikali kwa kuwagawia vyandarua pindi wanapokwenda kuanza kliniki ili ziwasaidie kujikinga na malaria.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Hamid Njovu.

Baadhi ya akina mama hao, Mwanaidd Issa, Reonia Kahigi, Teo Munjungu walitoa shukrani zao hivi karibuni wakati wakiwa kwenye kituo cha afya cha Zamzam kilichopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Mwanaidd amesema kwa kipindi chote ambacho amekuwa akibeba ujauzito amekuwa akipewa chandarua na hii ni awamu ya tatu ambapo mtoto wake wa kwanza alipokwenda kupima ujauzito alipatiwa chandarua na mtoto wa pili, hivyo na sasa ana ujauzito wa mtoto wa tatu na ameshapewa chandarua ambazo zinamsaidia yeye na watoto wake kujikinga na malaria.

“Naishukuruserikali kwa kutujari sisi wajawazito kiafya kwani wote tunajua kuwa kuna akina mama hawana uwezo wa kununua chandarua ni mdogo lakini tunapo pewa bure inasaidia sana kuepuka Ugonjwa hatari wa malaria,” amesema Mwanaidd.

Upande wake, Reonia amesema kuwa chandarua wanazopewa na serikali wanapokwenda kuanza kriniki zimekuwa Msaada mkubwa katika familia yake kwani hakuna mgonjwa wa Malaria.

“Jamani serikali inatujari kwakuona kuwa nasi akinamama wajawazito tunapata frusa hii ya kupewa chandarua kiurahisi hivyo niombde akinamama tunapopewa Neti tuzitumie vizuri zitufae na tusishambuliwe na maliaria,” amesema Kahigi.

Mjungu ameeleza kuwa serikali inawajari watu wake shida inatokea pale ambapo sisi tunaothaminiwa tunapewa vyandarua na kuvitumia kuanikia dagaa, kujengea uzio wa Bustani ya mbogamboga, pamoja na kujengea uzio wa kufugia kuku.

“Kwa jinsi hiyo mimi niombe erikali iendelee kutoa elimu maana bado inatakiwa kwa jamii Ili kuepuka kuharibika kwa matumizi ya vyandaru,” amesema.

Kwa upande wake Dk. Boniphace Kayegeji ambae ni mkuu wa kituo cha Zamuzamu amesema kuwa mama mjamzito anatakiwa kutumia chandarua kwa usahihi na kufuata maelekezo anayopewa kliniki ili kuepuka Ugonjwa hatari wa Malaria.

Kayegeji amesema kuwa mama mjamzito anatakiwa kupata mlo kamili ili mtoto awe na afya boro.

“Niwambie akinamama wajawazito kuwa mama kama unakinga hafifu Jua hata mtoto tumboni anakuwa dhaifu kitu ambacho ni hatari,” amesema Kayegeji.

Amesema wanaume wanatakiwa kuwasindikiza wake zao Kirinick Ili wapate elimu juu ya malezi ya mama wakati wa ujauzito ili kuepuka changamoto ambazo zinaweza kujiotokeza.

Kayegeji amesema kuwa: “Kuna wakati Akinamama wanapohudhuria kliniki huwa wanapewa dawa ambazo ni Folic Acid na Ferrous Sulphate pamoja na dawa za Malaria sasa usipokuwa mwaminifu kuhudhulia kira terehe uliyopangwa inakuwa changamoto kwa mtoto alieko tumboni.

“Akina mama niwaombe kuachana na dhana potofu kuwa kwenda krinick mapema eti ujauzito utatoka sikweli hapo kinachotokea nikujikuta unapata madhara makubwa tofauti ungewahi Ili uelimishwe usingepata changamoto,” amesema.

Naye Mganga Mkuu wa Manispaa ya Bukoba, Dk. Peter Mkenda amesema kuwa mama mjamzito haruhsiwi kutumia vileo vya aina yoyote ili kumuweka mtoto salama.

Amesema kuwa mama mjamzito hatakiwi kumeza madawa holera bila kuandikiwa na Daktari na madawa ya kulevya hayaruhusiwi pamoja na uvutaji wa sigara na bangi.

Ameongeza kuwa kipindi cha miaka mitano iliyopita maambukizi ya malaria yamepungua kutoka 7.0 hadi 5.4.

Pia Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Hamid Njovu amewashauri akina mama kufuata maelekezo wanayoyatoa watalam wa afya miezi mitatu kabla ya kupata ujauzito Ili kutambua utayari wao kiafya.

“Mama anapofata maelekezo ya wahudumu wa afya wakati wa ujauzito nakuacha mila potofu anakuwa na aslimia kubwa ya kujifungua mtoto mwenye afya bora,” amesema Njovu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles