25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

CAG kukagua mradi wa viwanja Manispaa ya Bukoba

KassimNa Mwandishi Wetu, Bukoba

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amemwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aende Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kufanya upya tathmini na kukagua ugawaji wa viwanja 843 kwenye manispaa hiyo.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo juzi, wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mayunga, mjini Bukoba.
Alifikia hatua hiyo baada ya wananchi kubeba bango lenye ujumbe kuelezea kutopewa viwanja hivyo vilivyopimwa na Manispaa ya Bukoba.

Viwanja hivyo vilipimwa na kugawiwa kwa wananchi ambao baadhi yao baada ya kulipa fedha hawajapewa viwanja hivyo, ikiwa ni takriban miaka zaidi ya 10.

Akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Kagera, Waziri Mkuu alilazimika kumpandisha jukwaani Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo, Wallace Karia, ili atoe maelezo ya nini kimekwamisha wananchi kupewa viwanja hivyo.

Katika maelezo yake, Karia alisema mwaka 2003, vilitengwa viwanja 843, kati ya hivyo 352 vilikuwa eneo la Kyabitembe, 137 Ihungo, Rwome na vingine 132.

Karia ambaye hana muda mrefu tangu ahamishiwe katika manispaa hiyo, alisema kumbukumbu za ofisi zinaonesha kuwa viwanja 182 wahusika hawajakabidhiwa na vingine 85 vilikuwa havijapimwa eneo la Kilimahewa na Kashai, huku kukiwa na vingine 5,000 vya mradi.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa walitarajia kuwalipa wananchi hao katika mwaka wa fedha 2016/17, kauli ambayo ilisababisha kelele kutoka kwa wananchi waliohudhuria mkutano huo wa Waziri Mkuu.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles