22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Tiba ya kisukari kutolewa bure

kigwangalla-559x520NA HERIETH FAUSTINE, DAR ES SALAAM

SERIKALI itaanza kutoa bure matibabu ya ugonjwa wa kisukari ili wananchi wengi waweze kufikiwa na huduma hiyo.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imesema licha ya serikali kukabiliwa na changamoto ya ufinyu wa bajeti, itahakikisha inatoa matibabu hayo.

Akizungumza katika mkutano wa tatu uliowakutanisha wataalamu wa ugonjwa wa kisukari kutoka nchi mbalimbali kujadili namna ya kupambana na ugonjwa huo, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigangwala, alisema hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa sera ya Afya inayoitaka wizara hiyo kutoa huduma ya matibabu ya ugonjwa wa kisukari bure.

Alisema wizara hiyo imekuwa na dhamana katika sera ya afya kutoa tiba bure kwa wagonjwa wa kisukari nchini ila kutokana na uwezo wa fedha kuwa mdogo wameshindwa kuwajibika katika kutoa tiba stahiki na kusababisha idadi ya wagonjwa kuongezeka.

“Tumeshindwa kutoa tiba, elimu, wataalamu wa ugonjwa huo na kuanzisha kliniki katika vituo vya kutolea huduma stahiki na kwa wakati kutokana na kutokuwa na uwezo huo.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ugonjwa wa Kisukari (TDA), Profesa Andrea Swai, alisema ugonjwa huo huweza kukaa mwilini kwa muda mrefu bila mhusika kujigundua na husababisha kuharibu, figo, macho pamoja na mishipa ya damu” alisema Profesa.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles