25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Makarani wa Sensa Kagera wanolewa

Na Renatha Kipaka, Bukoba

BAADHI ya Makarani Wakufunzi wa Sensa ngazi ya Wilaya mkoani Kagera wamesema maendeleo chanya yanatokana na usahihi wa taarifa zitakazokusanywa pindi zoezi la kuhesabu watu na makazi litakapofanyika Agosti 23, 2022.

Wakizungumza na na Mtanzania Digital mwishoni mwa wiki, ikiwa ni siku ya 17 tangu kuanza mafunzo ya uadilifu wa kuwa wakufunzi wa makarani watakaokuwa kwenye kata.

Mkazi wa Wilaya ya Muleba, Jackoson Msigati amesema kuwa Serikali imefanya kuamini makarani ambao wanategemewa kwenda kufundishia wengine ngazi ya kata ili kupata usahihi na weledi na kazi ya kupata idadi ya Wananchi.

“Niseme tu maelekezo yote ambayo tumepewa ni kuhakikisha taarifa zote za sensa zinakuwa na usahihi wake na Serikali itumie namba kufanya maendeleo,” amesema Msigati.

Amesema zoezi la sensa linafanyika kila baada ya miaka 10 ikiwa ni kutafuta jinsi gani wataweza kufikisha maendeleo kwa wananchi.

Karani na mkazi wa Kata ya Kagondo Manispaa ya Bukoba, Jane Novath amesema elimu ya utambuzi inajengwa kwa makarani itawafikia wananchi kwa kufuata miongozo ya madodoso kwa nadharia na vitendo.

“Kuna vitu vya kujinyima kutenda kwa kipindi chote cha kupewa elimu kwani hapa kinachotumika ndicho kitakachokwenda kutumika kwa vitendo wakati wa utekelezaji wa jukumu la sensa Agosti 23,” amesema Novath.

Afisa Tehama kutoka makao makuu, Elikana Joseph amesema mwaka huu zoezi litafanyika kwa mfumo wa kidigitali maeneo yote.

Ameongeza kuwa uwasilishaji wa taarifa utatumia njia mtandao katika ukusanyaji na kuzifikisha sehemu zinazotakiwa.

Mkufunzi wa sensa Taifa, Morice Nyatega amesema hatua iliyopo sasa ni kutoa mafunzo ya uelewa kwa makarani wanaoandaliwa kwenda kufundisha kufundisha wengine.

“Lengo kubwa la mafunzo ni kuhakikisha taarifa zote zinakusanywa ziwe na weledi mmoja kwa nchi nzima,” amesema Nyatega.

Aidha, amesema zoezi la kupata takwimu za wananchi nchini ni kulenga maendeleo na utambuzi wa idadi kamili nakuona ongezo la uhitaji wa mambo kwenye mazingira yanayokaliwa na wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles