25.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

PSPTB yatangaza matokeo ya mitihani ya 24, hesabu bado mwiba

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Masomo yanayohusisha hesabu yameendelea kuwa mwiba kwa wanafunzi wanaofanya mitihani ya Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) ambapo wengi wameendelea kutokufanya vizuri ikilinganishwa na masomo mengine.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akitangaza matokeo ya mitihani ya Bodi ya Mitihani ya 24 makao makuu ya Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa Alhamisi Julai 21, 2022 na Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB, Godfred Mbanyi wakati akitangaza matokeo ya mitihani ya 24 iliyofanyika Mei 24 hadi 27, mwaka huu.

“Wakurugenzi wa Bodi ya PSPTB chini ya Mwenyekiti wake, Jacob Kibona leo Julai 21, imeidhinisha na kutangaza matokeo ya mitihani ya 24 katika ngazi mbalimbali za masomo ya bodi, katika matokeo haya watahiniwa waliojiandikisha kufanya mitihani walikuwa ni 1,031 lakini walioweza kufanya mitihani walikuwa ni 971 na kati ya hao, watahiniwa 458 sawa na asilimia 47.2 wamefaulu mitihani yao, watahiniwa 457 sawa na asilimia 47.1 wamefaulu baadhi ya masomo na watahiniwa 56 wao wamefeli kabisa na watatakiwa kurudia mitihani yao kwa ujumla.

“Tathmini inaonesha kwamba katika mitihani hii ya 24 kuna baadhi ya masomo yamefanyika vizuri na watu wamefaulu vizuri na masomo hayo yalikuwa sita, lakini kuna masomo machache hasa yale ambayo yanahusisha hesabu kumekuwa na changamoto sana kwa watahiniwa wa bodi kutokufanya vizuri asomo hayo,” amesema Mbanyi.

Mbanyi ametaja moja ya sababu inayochangia watahiniwa wengi kutokufanya vizuri katika matokeo hayo ni kujiamini sana kupita kiasi.

“Uchunguzi unaonyesha kwamba watahuniwa wengine wamekuwa wakijiamini sana kiasi kwamba wamekuwa hawahudhirii masomo kwenye vituo vya bodi na mwisho wa siku wanapokuja kufanya mitihani wanafeli.

“Wale wote wenye mitihani ya marudio wanatakiwa kijiandaa vizuri kwa mtihihani yao ya mwezi wa 11 ili waweze kufahulu vizuri, pia kwa wale wote wanaotarajia kufanya mitihani ya bodi wanatakiwa kuhudhuria kwenye vituo vya kujiandaa na mitihani maana changamoto ni kuwa vijana wanajiamini kupita maelezo na kuvibeza vituo hivyo na kusababisha kufanya mitihani ya bodi bila kuhudhuria vituo ambavyo vimesajiliwa na bodi hiyo,” amesema Mbanyi.

Aidha, amesema watahiniwa wote wanaweza kumtazama matokeo yao kupitia tovuti ya bodi ya www.psptb.go.tz na pia matokeo hayo yatatumwa kwenye akaunti ya kila mtahiniwa ili kurahisiha upatikanaji wa tokeo yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles