26.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Jela miaka 20 kwa kosa la kupatikana na nyara, silaha za hifadhi

Na Malima Lubasha, Serengeti

Mahakama ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, imemhukumu kwenda jela miaka 20, Samson Matungi(31) mkazi wa kijiji cha Nyamburi wilayani hapa baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kupatikana na silaha pamoja na nyara za Serikali kinyume cha Sheria.

Akisoma hukumu hiyo Juni 30, 2022, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Jacob Ndira amesema ametoa adhabu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa bila kuacha shaka yoyote.

“Mahakama inakutia hatiani mshtakiwa hivyo ninakuhukumu kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka 20 jela, ili iwe onyo na fundisho kwa watu wengine wanaojihusisha na ujangiri katika Hifadhi za Taifa, kwani tabia hiyo zinahujumu uchumi wa nchi,” amesema Hakimu Ndira.

Amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo Novemba 8, mwaka jana ndani ya eneo la Nyamburi lililo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambapo alikutwa akifanya ujangiri.

Katika kesi hiyo namba 170 ya mwaka 2021, upande wa Jamhuri ukiongozwa na Mwendesha Mashtaka Wakili wa Serikali, Josephat Jakinila umedai mshtakiwa alikutwa na kosa la kuwa na panga moja, nyara za serikali ambazo ni shingo iliyoungana na kichwa ya mnyama nyamela yenye thamani ya Sh milioni 1.84 ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria.

Awali, upande wa Jamhuri uliomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili liwe fundisho kwa watu wengine wanaojihusisha na vitendo vya ujangiri kwani vinarudisha nyuma jitihada za serikali  za kuhifadhi maliasili zetu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles