29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kuanzisha chaneli ya Kilimo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde amesema serikali iko mbioni kuanzisha chaneli ya kilimo kupitia Televisheni ya Taifa (TBC), itakayokuwa inatoa elimu ya kilimo na taarifa za mazao.

Katika elimu ya kilimo elimu itakayotolewa itahusu kanuni bora za kilimo, maeneo ya uwekezaji na fursa mbalimbali za kilimo.

Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo.

Mavunde amesema hayo leo Februari 23, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akizindua kipindi maalumu cha Kilimo kwanza kitakachokuwa kinarushwa na kituo cha Televisheni cha TVE kwa lengo la kuhamasisha kilimo miongoni mwa vijana na kutoa taarifa muhimu za kilimo.

“Nawapongeza sana TVE kwa wazo hili la kuamua kuunga mkono jitihada za serikali za kukuza kilimo nchini. Kipindi hiki kitasaidia kuhamasisha matumizi ya sayansi na kanuni bora za kilimo ili wakulima wetu walime kwa tija.

“Pia kipindi hiki cha Kilimo Kwanza cha TVE kitakuwa kinaongeza taarifa na maudhui zaidi ya kilimo ambayo tutayarusha kupitia TBC kwenye chaneli ya Kilimo ambayo tunatazamia kuianzisha hivi karibuni itakayojikita kutoa elimu kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ikiwa ni pamoja na mafunzo ya kanuni bora za kulima na matumizi sahihi ya pembejeo kwa wakulima,” amesema Mavunde.

Awali Ofisa Mtendaji Mkuu na Mmiliki wa Kituo cha Radio EFM naTVE, Francis Sizza maarufu Majizzo amesema lengo kuu la kipindi hicho ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kukuza kilimo.

“Kupitia kipindi hiki, tumejipanga kuhakikisha tunawahamasisha vijana wa vijijini na mijini wakiwamo wasanii wakubwa wa muziki na filamu nchini
kushiriki katika kilimo kama sehemu ya kampeni ya kunufaika na mpango wa serikali wa Building a better tomorrow, Toboa na Kilimo,” amesema Majizzo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles