32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Bilioni 200 za NMB kuwatajirisha Machinga nchini

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

UMOJA wa wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama Machinga Tanzania wamesema bilioni 200 zilizotengwa na benki ya NMB siyo tu zinakwenda kuwasaidia kwenye mitaji yao, bali zinawavusha kutoka kwenye umasikini na kuwa matajili.

Kauli hiyo ilitolewa leo Februari 23, 2022 na Mwenyekiti wa Machinga, Elias Matondo katika mkutano wa wafanyabiasha hao unaonedelea jijini Dodoma.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa Machinga kutoka mikoa yote Tanzania Bara na kuwashirikisha viongozi wa Serikali kwa Wizara za Tamisemi na Maendeleo ya Jamii likiwemo jeshi la Polisi.

Lengo la mkutano ni kuwekana sawa katika kujadili changamoto zinazowakabili Wamachinga na kuzipatia ufumbuzi na mfadhiri wa mkutano ilikuwa benki ya NMB.

Matondo alisema kutengwa kwa fedha hizo kutoka benki ambayo wanaiamini kumewapa faraja kubwa na tumaini la kuwa sasa wanakwenda kuacha kuitwa machinga badala yake wanatengeneza utajiri.

Alisema kwa muda mrefu walikuwa wakiishi kama njiwa asiye na kiota hata mara kadhaa walipotaka kufanya mikutano walishindwa kufanya kwani hawakuwa na fedha lakini tumaini jema ni kuwa wamepata mtu wa kuwashika mkono.

“Kwa niaba ya wenzangu nasema asante sana Serikali, lakini shukrani zangu zielekee kwa NMB, kuna wakati tulifanya mkutano kidogo tuishie kwenda jela lakini hata mkutano huu wamefadhiri wao na mambo yanakwenda vizuri amani kwa kila mtu,” alisema Matondo.

Akizungumza nje ya ukumbi Ofisa wa NMB, Martine Massawe alisema banki hiyo imeanzisha utaratibu mzuri wa namna bora ya kuwainua wamachinga nchini huku akisisitiza kuwa miaka mitano itakuwa ya ukombozi kwao.

Massawe alisema wameingia mkataba na wafanyabiashara hao kw akushirikiana na Serikali ambapo Sh200 bilioni zimetengwa kwa ajili ya yao na zitatolewa kwa mpangilio mzuri wa ushirikishwa ili wasijipenyeze wasiostahili.

Kwa mujibu wa Massawe, kutakuwa na akaunti maalumu kwa ajili yao na wameweka utaratibu ambao utakuwa ukiwatambulisha kila tawi watakalokwenda ili wasiingie kwenye foleni ya kuwachelewesha.

“Siyo hilo tu, lakini tumewaletea mambo mazuri ikiwemo hata bima yay a fao ambapo mtu atakata kwa Sh 10,000 kwa mwaka lakini inapotokea tatizo anaweza kulipwa hadi Sh 500,000 yote hayo tunalenga kuwakuza,” alisema Massawe.

Alisema nia ya NMB ni kuona Machinga wakibadilika na kukua kutoka hali ya chini kwenda kipato cha kati hadi kikubwa ambapo nao watafikia kuitwa matajili kwa kuwa hata wenye fedha walianzia chini.

Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Makundi maalumu Dk. Zainabu Chaula aliwataka wamachinga nchini kote kutumia fursa ambayo imetolewa na mabenki ikiwemo NMB ili kukuza mitaji yao na kuachana na biashara za kukimbizana.

Dk. Chaula alisema si vema na haki mtu kufanya biashara hiyo hiyo kwa miaka yako bila kubadilisha lakini kama ilishindikana ni kutokana na kukosa mitaji hivyo iwezekane kupitia fursa iliyotolewa na NMB.

Katibu huyo alisisitiza suala la uaminifu pindi watakapoanza kupewa mikopo hiyo kuwa ndicho kitu kitakachowapambanua na wengine kubakia nyuma kwa kuwa fedha zinahitaji kuwa kwenye mzunguko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles