26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Simba kuivaa Singida United Kombe la FA

kikosi cha simba (2)NA ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM

TIMU ya Simba kesho itashuka dimbani kucheza mchezo wao wa hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Singida United katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba ilipiga hatua moja mbele baada ya kuitoa Burkina Faso ya Morogoro kwa kuinyuka mabao 3-0 katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Simba ambayo ina machungu ya kupoteza mchezo wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga  baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-0, hivi sasa  inaendelea na maandalizi yake katika Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini, Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi, kocha wa timu hiyo, Jackson Mayanja, alisema amekiandaa kikosi chake kuhakikisha kinapata ushindi  ili kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Alisema katika mchezo huo timu yake itaingia uwanjani kivingine huku ikiwa na lengo moja la kupata ushindi wa mabao mengi ambayo yatawasaidia mbele ya safari.

“Licha ya kufanya marekebisho kwa mapungufu niliyoyaona lakini pia mchezo utanisaidia kugundua mengine yaliyojificha ili niendelee kuyarekebisha kwani tunahitaji kutwaa ubingwa wa michuano hii pamoja na kumaliza ndani ya nafasi mbili za juu kwenye Ligi Kuu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles