22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

‘Cannavaro’ ampa mtihani Pluijm

canavaro plujimNA ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM

BEKI wa Yanga na nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amesema suala la yeye kupata namba katika kikosi hicho lipo mikononi mwa kocha wake, Hans van de Pluijm.

Cannavaro amekuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili akiuguza majeraha aliyoyapata wakati akiitumikia timu ya taifa ‘Taifa Stars’.

Lakini tangu ajiunge na wenzake takribani wiki tatu sasa hajafanikiwa kupata namba kwenye kikosi cha Pluijm baada ya wachezaji chipukizi kuonekana kumzidi uwezo.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi, Cannavaro alisema kwanza anafurahishwa kuona hivi sasa kuna warithi wake katika kikosi chao tofauti na ilivyokuwa awali.

Alisema uwepo wa wachezaji chipukizi kama Pato Ngonyani ambao wanaonyesha ustadi mkubwa wa kulinda ukuta kunampa matumaini kuwa hata kama ataamua kuachana na soka leo bado Yanga itakuwa na kikosi imara cha ushindani.

“Nafurahi kuona kuna vijana wanaweza kuniweka benchi, sioni wivu kwa hilo kwani nina nafasi kubwa Yanga, muda wowote kocha akinipa nafasi ya kucheza nitafanya kazi yangu.

“Unajua mchezaji hawezi kujipangia majukumu ila napangiwa na benchi la ufundi na mimi ni sawa na wengine, naweza kusema hatima yangu kwenye kikosi cha Yanga ipo mikonini mwa kocha wangu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles