Safina Sarwatt, Same
Katika kuadhimisha miaka 45 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Same mkoani Kilimanjaro kimeshiriki kufanya shughuli za kuchimba msingi wa ujenzi wa jengo la ofisi ya Chama itakayo gharimu zaidi ya Sh milion 175.
Mkuu wa Wilaya Same, Edward Mpogolo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi ameongoza zoezi hilo ambapo amesema tangu kuanza kwa Wilaya hiyo CCM hajiwahi kuwa na ofisi yenye hadhi ya wilaya.
Amesema ofisi iliyopo kwasasa ni ndogo na kwamba haina hadhi ya kuwa ofisi ya chama kubwa ambayo inaongoza dola na dhamira yao ni chama hicho kujitegemea.
Katibu wa wilaya ya Same, Hamisa Chacha amesema jengo hilo pia itatumika kama kitega uchumi cha chama ili kiweze kujiemdesha.
“Ujenzi wa jengo hilo ni pamoja na kuweka fremu za biashara ili chama kiweze kujiingizia kipato na kujiendesha kwa mapato yake yenyewe,”amesema.
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Same Isaya Juma amesema kuwa kukamilika kwa jengo hilo itasaidia kupunguza msongamano katika watumishi wa chama hicho ambapo kwasasa jumuiya za chama hicho wanaitumia ofisi moja.
Hizo fedha wamezitoa wapi?