25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Watoto, vijana wapendekeza kuwapo kwa Maofisa Ustawi wa Jamii shuleni

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Kukosekana kwa Maofisa Ustawi wa Jamii shuleni imetajwa kuwa ni moja ya chanzo cha changamoto nyingi zinazowakabili watoto na vijana kutokana na kukiosa mtu wa kumshirikisha mawazo yao.

Hayo yamebainishwa Oktoba 9, 2021 jijini Dar es Saalam na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la REPSSI Tanzania, Edwik Mapalala wakati wa Warsha ya kujadili changamoto za zinazowakabili watoto ikiwa ni maandalizi ya mkutano mkuu wa mwaka utakaoanza Oktiba 13-15 nchini Msumbiji ukihusisha nchi 13 Tanzania ikiwemo.

Ibrahim Kalambaga(Kushoto) akiwasilisha changamoto za Watoto na Vijana wa Tanzania, kulia ni Mkufunzi Msaidizi kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii(ISW), Rukia Mwinyi.

Amesema upande wa Tanzania changamoto zilizowasilishwa na watoto pamoja na vijana ni pamoja na shule kutokuwa na maofisa ustawi wa jamii ikilinganishwa na nchi nyingine badala yake una walimu wa maelezi ambao wamekuwa wakielemewa na majukumu ya kufundisha.

“Pamoja na kwamba walimu wamekuwa wakifanya kazi nzuri ya kuwafundisha watoto, lakini ni bayana kwamba kukosekana kwa maofisa ustawi wa jamii maeneo ya shule imekuwa ni moja ya changamoto jambo ambalo linasababisha watoto kukosa msaada wa kisaikolojia pale wanapopata changamoto.

“Watoto wanaona kama wamekuwa wakikosa mahala pa kukimbilia na ndio maan wanapendekeza kuwapo kwa walimu hawa, hatua itakayopunguza changamoto, jambo hili limekuwa likifanywa na majirani zetu hasa kwenye shule za binafasi hivyo tunaamini iwapo litafanyiwa kazi na hapa kwetu kama walivyopendekeza watoto basi litakuwa na matokeo chanya,” amesema Mapalala.

Washiriki wa Warsha hiyo wakiendelea na majadiliano.

Mapalala amesema mbali na changamoto hiyo pia watoto hao wamegusia ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi na kwamba bado wazazi hawaoni umuhimu wa kuongea na watoto wao juu ya jambo hilo muhimu.

“Watoto wanaona kuwa bado kuna usiri ulipo kutoka kwa wazazi ambao wamekuwa hawapi elimu juu ya afya ya uzazi hatua inayochochea kukosa elimu sahihi yakuweza kuwaepusha na vishawishi vya dunia ya sasa ilivyo,” amesema Mapalala.

Mapalala amesema Repssi limekuwa likikutanisha watoto na vijana kwa ajili ya kujadili changamoto mbalimbali za afya ya akili.

“REPSSI tumekuwa na kawaida ya kila baada ya miaka miwili kukutanisha watoto na vijana wakiwamo watu wazima kwa ajili ya kujadili afya ya akili lengo likiwa ni kuhimiza familia na jamii kuangalia ustawi wa kisaikolojia kwa mtu mmoja mmoja na watoto.

“Kwani tunaamini kwamba ustawi wa kisaikolojia wa mtoto au kijana unapoimarishwa tunajenga taifa la watu wanaoweza kuwajibika ipasavyo, hivyo mkutano wetu mwaka huu kauli mbiu imejikita kwenye kuhakikisha kuwa tunakuwa wabunifu, kujumhisha vijana na watoto kwenye mikakati mbalimbali ili waweze kuendelea kwenye muktadha uliobora,” amesema Mapalala na kuongeza kuwa wao wamekuwa wakihimiza mtazamo wa kila moja kumjali mwenzake ikiwa ni pamoja na kuacha ubinafsi ili kuleta amani.

“Mahitaji ya afya ya akili na msaada wa kisaikolojia ni muhimu sana katika jamii, hivyo ukiona mwenzako ana tatizo jitahidi kumsaidia,kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla,” amesema Mapalala.

Mkufunzi Msaidizi kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii(ISW), Rukia Mwinyi(Kushoto) akifuatilia majadiliano hayo.

Upande wake, Karesma Mushi ambaye ni Afisa Miradi wa Repssi Tanzania akizungumzia warsha hiyo ya siku mbili iliyokutanisha watoto na vijana wa Tanzania na wenzao wa mataifa 12 kutoka Kusini na Mashariki mwa Afrikaamesema kuwa lengo ni kuandaa ajenda watakazoenda nazo kwenye mkutano mkuu.

“Hii ni warsha ya maandalizi kuelekea kwenye mkutano mkuu utakaofanyika Oktoba 13 -15 Maputo Msumbiji ikihusisha nchi 13, hivyo hapa tunajadili masuala yanayowahusu ambayo yamegawanywa katika nyanja tano ikiwamo ukatili wa kijinsia na kwa watoto, ulinzi kwa vijana na watoto, elimu, uchumi na uviko-19 kwa namna yalivyoathili watoto.

“Tumepata changamoto mnbalimba;pi za watoto ikiwa ni pamoja na kukabiliana na ukatili wa kingono wakati wa janga la corona ikiwamo udhalilishaji.

“Ikumbukwe mkutano huu unatuwezesha kukusanya maoni ya watoto kwa nchi zote 13 ambayo yatawasilishwa kwenye siku ya mkutano mkuu Oktoba 13,” amesema Karesma.

Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo kutoka maeneo mbalimbali wakifuatilia majadiliano.

Moja ya vijana waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Ibrahim Kalambaga ambaye alisema kuwa wanahitaji kuona vijana wakipatiwa huduma rafiki ikiwamo uhuru wa kufanya machaguo yao wenyewe kwenye maisha.

“Vijana tunakabiliwa na changamoto nyingi kwani tunatamani kuona tukipata elimu ya afaya ya uzazi, kupatiwa maofisa ustawi wa jamii kwenye maeneo ya shule ambao watakuwa msaada kwa wanafunzi wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwamo za kimazingira,” amesema Kalambaga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles