23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Soko la filamu ‘linavyolindwa’ kikatili Korea Kaskazini

Hassan Daudi na Mashirika

KOREA Kaskazini ina sheria iliyotafsiriwa na mamlaka za nchi hiyo kuwa ni mkakati wa kulinda soko la filamu za ndani.

Sheria hiyo mpya ya Korea Kaskazini imeweka adhabu kali dhidi ya raia wa nchi hiyo atakayekutwa na filamu za nje. Iwe ameibeba kwenye ‘CD’ au kifaa kingine chenye uwezo wa kubeba ‘muvi’.

Kwamba ni adhabu ya kifo na si kingine kwa raia wa Korea Kaskazini atakayekutwa na mzigo wa filamu zinazotoka nje (Marekani, China, Korea Kusini, Japan n.k.). Hiyo ni kwa aliyekutwa na mzigo, kwa maana ya mfanyabiashara.

Kwa aliyekutwa akitazama, mathalan kama inavyokuwa ukiwa umetulia nyumbani kwako, adhabu yake ni kutupwa gerezani kwa kipindi cha miaka 15. Kwanini sheria hiyo? Kama ilivyotanguliwa kusema katika aya ya kwanza ya makala haya, Serikali ya Korea Kaskazini ilikuja na mpango huo baada ya kuona nchi yao imekuwa ‘jalala’ la filamu za kigeni, zikiwamo za mahasimu wao, Korea Kusini na Marekani.

Mathalan, miaka 20 iliyopita, filamu iitwayo ‘Stairway to Heaven’ ya Korea Kusini ilikuwa umaarufu kila kona ya Korea Kaskazini. Kama hiyo haitoshi, kwa mwaka 2002 pekee, ulifanyika upekuzi katika chuo kikuu kimoja na kukutwa ‘CD’ zaidi ya 20,000 za filamu za kigeni.

Korea Kusini haitakiwi kabisa Vyanzo vya makala fupi haya vinadai kuwa ni bora raia wa Korea Kaskazini anayekutwa akitazama filamu ya China kuliko anayekodolea macho ‘muvi’ ya Korea Kusini.

“Mtu anayetazama video za China atapata adhabu ndogo, ukilinganisha na anayetazama zile za Korea Kusini,” kinasimulia chanzo hicho. Kwa upande wake, Yoon Mi-so ambaye ni raia wa Korea Kaskazini, anakumbuka alivyowahi kushuhudia mtu akiuawa baada ya kukutwa na mzigo wa filamu za Korea Kusini.

Anasema siku ya kuuawa, majirani walitakiwa kushuhudia ili iwe fundisho. “Kama ungekataa kwenda, basi ungeshitakiwa kwa uhaini,” anasema Mi-so.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles