29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Bonnah awataka wananchi kuacha kujenga kwenye hifadhi ya barabara

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kamoli, amewataka wananchi wa Mtaa wa Msingwa Kata ya Bonyokwa kuacha kujenga kwenye hifadhi ya barabara ili wasikwamishe miradi ya maendeleo.

Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kamoli (katikati) akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Msingwa baada ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero zao. Kulia ni Diwani wa Kata ya Bonyokwa, Tumike Malilo.

Bonnah ambaye anaendelea na ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi katika mitaa na kata mbalimbali za jimbo hilo, amesema baadhi ya wananchi wamejenga kwenye hifadhi ya barabara suala ambalo huleta ugumu kufikisha miradi ya maendeleo.

“Kama huku Msingwa watu wamejenga mpaka barabarani ukisema unaleta greda huku utalipitishaje…jamani nawaomba tuache barabara ni kwa faida yetu sote,” amesema Bonnah.

Aidha amewaagiza wenyeviti wa serikali za mitaa kutoa elimu kwa wananchi ili wanapojenga wakumbuke kuacha barabara.

Mbunge huyo pia alikagua barabara ya Kwa Makofia ambapo kupitia mfuko wa jimbo zimetolewa Sh milioni 5 kwa ajili ya kuikarabati iweze kupitika. Hata hivyo amesema itajengwa kwa kiwango cha changarawe na kuwekwa mifereji ili iweze kupitika wakati wote.

Akikagua kivuko kinachounganisha Mitaa ya Msingwa na Khanga amesema kinatarajiwa kuanza kujengwa hivi karibuni na tayari Sh milioni 15 zimetolewa.

Pia alikagua barabara iliyopo eneo la Kwa Mjumbe Nyoka na kusema kuwa wakati wanasubiri mradi wa DMDP uanze atashirikiana na diwani kuikarabati iweze kupitika.

Kuhusu kero ya maji mbunge huyo amewahakikishia wananchi hao kuwa maeneo ambayo hayajapata juhudi zinafanyika kwa kushirikiana na Dawasa na hivi karibuni maji yatafika.

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Msingwa, Hassan Ng’imbi, amesema wakati wa mvua wananchi wamekuwa wakipata adha kubwa kutokana na barabara nyingi kutopitika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles