24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

Kumbilamoto aitaka jamii kuchangamkia fursa benki ya TCB

Na Jestina Zauya (TUDARCo), Mtanzania Digital

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto ameipongeza Benki ya Biashara Tanzania (TCB) kwa kuendelea kusogeza huduma karibu na wananchi na kuitaka jamii ichangamkie fursa zinazotolewa na benki hiyo.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto, akikata keki kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja katika Benki ya Biashara Tanzania (TCB) Tawi la Mbagala. Kulia ni Meneja wa Tawi hilo, Edward Moleka na Watatu kushoto ni Diwani wa Kata ya Charambe, Twahil Kamona.

TCB ambayo ni benki ya Serikali ni zao la iliyokuwa Benki ya Posta (TPB) na Benki ya Maendeleo (TIB) ilizinduliwa rasmi Julai mwaka huu.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja yaliyofanyika katika benki ya TCB tawi la Mbagala, amesema kwa muda mfupi benki hiyo imefanya mabadiliko makubwa.

“Ninyi mmeminika katika jamii ndiyo maana mmebebeshwa mzigo mkubwa wa benki nyingine zilizounganishwa, mmenithibitishia kuwa faida mnayopata mnaitumia kutatua changamoto mbalimbali za kijamii nawapongeza lakini nawashauri kwakuwa mko katika Kata ya Mbagala muipe kipaumbele”, amesema Kumbilamoto.

Aidha ametoa wito kwa jamii kuitumia benki hiyo kwani riba zake ni nafuu ukilinganisha na benki nyingine.

Naye Msimamizi Mkuu wa Matawi ya TCB Tanzania, Godfrey Numuhanga, hivi sasa benki hiyo imekuwa ni kimbilio la wananchi wengi kwa sababu ni benki kubwa ya Serikali ambayo huduma zake ni kisasa na zinashindana na benki nyingine.

Amesema pia dirisha la wanawake bado wanaliendeleza na kwamba wanatarajia kutoa mikopo mingi kuwezesha wanawake wajasiriamali walioko kwenye vikundi na mtu mmoja mmoja.

“Tumeamua kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kuwaonyesha upendo wateja wetu na kuwashukuru kwa kutumia huduma zetu,” amesema Nyamuhanga.

Kwa upande wake Meneja wa TCB Tawi la Mbagala, Edward Moleka, amesema wamekuwa wakirudisha sehemu ya faida kwa wateja wao kwa kusaidia kutatua changamoto mbalimbali kama za afya na elimu.

“Tunasaidia watoto yatima lakini pia tuna miradi mikubwa ya kujenga shule, vituo vya afya na tutaendelea kufanya zaidi kwa wananchi wanaoiunga mkono benki yetu na wale ambao watakuja kuwa wateja baadaye,” amesema Moleka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles