25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Ubunifu waongeza ushindani sekta ya Bima

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni ya Bima ya Phoenix Issurance imezindua huduma ya Utulivu kwa lengo la kuwasaidia wateja wao wanapopata matatizo mbalimbali wakiwa kwenye vyombo vyao vya moto (magari).

Afisa Mtendaji Mkuu wa Phoenix, Ashraf Musbally amesema kuwa huduma hiyo ni ya bure kwa wateja wao wa bima kubwa ya magari (comprehensive).

Musbally alisema kuwa wamiliki wa vyombo vya moto wanakutana na changamoto nyingi ikiwa kama kuharibikiwa na magari, kupata pancha, kuishiwa mafuta, kusahau funguo na nyinginezo ambazo wao watazifanya bila ya gharama yoyote.

“Lengo la kutoa huduma hii ni kuwapa utulivu wateja wetu wanapokabiliana na matatizo mbalimbali wakiwa barabarani na hata nyumbani kwao.
Unaweza kukuta gari lako limepataa kuwaka, unachotakiwa kufanya ni kutoa taarifa kwetu na mafundi watakuja kufanyia matengenezo hapo hapo nyumbani kwako,” alisema Musbally.

Alisema kuwa  mipango yao ni kutoa huduma hii mikoani kwa wateja wao hata wa mikoani katika siku za hizi karibuni.
 
“Hii ni huduma ya ziada, haina malipo yoyote ambapo mteja wetu wa bima kubwa atafaidika nazo, nawaomba wateja wetu wa bima nyingine kufanya.

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Phoenix Assurance Robert  Kalegeya amesema kuwa wameamua kutoa huduma hiyo kama kuwafariji wateja wao ili waendelee kufanya nao kazi.

Bw Kalegeya alisema kuwa biashara ya bima ina ushindani mkubwa  kutokana na uwepo wa makampuni mengi hapa nchini.

Alisema kuwa kutokana na ushindani huo, kampuni yao imeamua kuwa na ubunifu wa kutoa huduma mbalimbali ili kutoa huduma bora kwa wateja wao.

Meneja wa Leseni na Usimamizi wa mwenendo wa soko wa mMamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Tanzania (TIRA) Hillard Maskini aliipongeza kampuni hiyo ya Bima kwa kuanzisha huduma hiyo bora kabisa.

Kwa upande wa Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma cha Trafiki Makao Mkuum Mrakibu wa Jeshi la Polisi Mossi Ndozero alisema kuwa huduma hiyo ina lengo la kudumisha usalama wa wateja ambao jeshi la Polisi linasisitiza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles