Na Mwandishi Wetu
Timu ya Simba imetoka suluhu na Biashara United katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/2022,huku Ruvu Shooting ikikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Dodoma Jiji FC.
Mchezo wa Wekundu wa Msimbazi hao umepigwa leo Septemba 28, 2021 kwenye dimba la Karume, Musoma, wakati Ruvu Shooting ilikuwa mgeni wa Dodoma Jiji Uwanja wa Jamhuri , Dodoma.
Bao pekee lililoipa ushindi Dodoma Jiji dhidi ya Ruvu Shooting limefungwa na Clephace Mkandala dakika ya 33.
Mchezo mwingine wa ligi hiyo, Mbeya City imeanza vizuri baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya maafande wa Tanzania Prisons bao lililofungwa na Peter Mapunda kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.