23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Kagera waomba chanjo ya Covid -19 itolewe bila masharti

Na Renatha Kipaka, Bukoba.

BAADHI ya wananchi mkoani Kagera wametaka  chanjo ya Covid -19 itolewe bila masharti kama  nyingine ili  kuwaondolea hofu.

Mmoja wa wananchi hao, Teresia Mgisha (40) ambaye ni mfanyabiashara wa ndizi na mkazi wa Kayanga amesema  kuwa mama yake alipochanjwa katika awamu ya kwanza alimsimulia mashariti yaliyoko kwenye fomu ambayo yalimfanya  aogope.

“Niseme tu kwa upande wa wawanake wanajua tunapo jifungua huwa watoto tunawapereka hospitalini wanapata chanjo na hatuna hofu kabisa sasa kwa hili mashariti yanatisha kabisa,”anasema Teresia.

Naye Teresifori Gaspar (50) mkazi wa Bukoba Mjini anasema shida kubwa ya zoezi la chanjo ya Corona  ni  kukosa elimu ya kutosha kutoka kwa wahudumu wa afya.

Amesema  kuna  watu wengine ili wachukue hatua ya kuamini chanjo  hadi  wamuone mtu alievaa vazi jeupe vinginevyo ni ngumu sana kuelewa.

“Niombe  Serikali  kupitia Wizara ya Afya kuwatumia  wauguzi kutoa elimu kwa wananchi,  itasaidia watu kuelewa,”anasema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Waganga Wakuu wa Wilaya zote mkoani Kagera Dk. Diocles Ngaiza  alipozungumza  katika kikao cha msingi cha Kamati ya Afya ya Mkoa Kagera kuwa  Halmashauri ya Kyerwa ilipatiwa chanjo 5000  na hadi  Septemba  27, wamechanjwa  watu 1742 ambapo watumishi wa afya ni  217 na ambao wamechanjwa ni 129 ambapo nisawa sawa na asilimia 59.

“Jambo la Msingi  ni kutoa elimu mfano katika Halmashauri yetu ya Kyerwa tumeweka makubaliano ya pamoja kuwa ifikapo 1 Oktoba watumishi wote wa Afya wawe wamechanjwa “amesema  Ngaiza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles