Na Brighiter Masaki,Mtanzania Digital
Chama cha mchezo wa Karate Tanzania (TASHOKA) mwishoni mwa wiki hii kinatarajia kuendelea na mashindano ya Ndondo Karate Championship katika maeneo ya Ilala Boma, Jijini Dar Es Salaam.
Mashindano hayo yenye lengo la kukuza vijana wa mchezo huo kuanzia ngazi ya chini ya mchezo huo na hatimaye hapo baadaye vijana hao kuiwakilisha Tanzania katika michuano mbalimbali.
Akizungumza na Mtanzania Digital, Mwenyekiti wa TASHOKA Sensei Yahaya Mgeni amesema aina ya mashindano hayo yanafanyika katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania.
“Hii ni mara ya kwanza kufanyika kwa aina hii ya mashindano nchini Tanzania na pia chama cha mchezo wa karate kina mpango wa kuwatumia mabingwa wa mashindano hayo katika mashindano ya Nyerere Day Oktoba 10, mwaka huu.
“Baada ya mashindano hayo, baadaye kutakuwa na mashindano ya makarateka wazoefu wa mchezo huo kwa lengo la kuzidi kuufanya mchezo huo kukua nchini Tanzania,”amesema.