30.3 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Kujengewa uwezo kulivyo okoa uharibifu wa misitu Same

Na Mwandishi Wetu, Same

Kujengewa uwezo wa kuendesha miradi rafiki ikiwemo ufugaji samaki na utengenezaji majiko banifu kwa wananchi, umesaidia kupungua uharibifu wa misitu uliokuwa ukifanywa ndani ya hifadhi ya Mazingira asilia ya Chome iliyoko wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro.

Kijiji cha Mbakweni kilichopo katika kata ya Msindo ni miongoni mwa vijiji ambavyo kupitia kikundi cha Wanawake wanatekeleza miradi wa utengenezaji wa majiko banifu na ufugaji wa samaki.

Wakizungumza hivi karibuni wanufaika hao wamesema mradi huo waliowezeshwa na Mfuko wa Uhifadhi wa Milima ya Tao la Mashariki (EAMCEF) kupitia Shirika la SMECAO linaloshughulika na uhifadhi wa Mazingira Wilaya za Same na Mwanga imekua mkombozi kwao katika kujiongezea kipato na kuboresha lishe.

Mmoja wa wanakikundi hao, Roida Manase, amesema mbali na kuboresha kipato na lishe miradi hiyo pia imewapunguzia safari za msituni walipokuwa wanakwenda kwa ajili ya kuvuna miti ya mbao na  kuchoma mkaa lakini pia teknolojia ya matumizi ya majiko banifu imepunguza matumizi ya kuni na kuwaongezea muda wa kufanya shughuli nyingine.

Akieleza lengo la kusaidia uhifadhi wa hifadhi hiyo ya Mazingira asilia ya Chome na kuwashirikisha wananchi,Afisa wa miradi wa EAMCEF Kanda ya Kaskazini,Magret Victor amesema ni ili kulinda bionuwai zilizopo ndani ya hifadhi hiyo kutokana na umuhimu wake .

“Hifadhi hii ya mazingira asilia ya Chome ina utajiri mkubwa wa bioanuwai lakini pia ndio chanzo kikuu cha maji yanayotegemewa na wananchi wanaoishi milimani na maeneo ya tambarare hivyo inahitaji nguvu kubwa ya kuitunza kwa maendelo endelevu,”ameongeza

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Same ambaye pia ni  mjumbe wa kamati ya ushauri wa miradi inayotekelezwa na EAMCEF wilayani humo, Yusto Mapande, ameeleza miradi hiyo inatekelezwa wakati muafaka ambao hifadhi hiyo ilikua kwenye kiwango kikubwa cha uharibifu

Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2015 Mfuko huo umetoa zaidi ya Sh Milioni 90 kwa SMECAO kwa ajili utekekezaji wa miradi ya majiko banifu na ufugaji wa samaki kwa lengo la kukuza kipato cha wananchi na kuhifadhi mazingira wilayani humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles