23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Muriya Oman yazindua maonyesho ya makazi ya kisasa Dar, Zanzibar

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya Muriya ambayo inajishughulisha na mradi mkubwa wa makazi nchini Oman, imehitimisha  maonyesho yake ya kila mwaka ya makazi visiwani  Zanzibar na sasa maonyesho hayo yanahamia jijini Dar es Saalam.

Meneja wa miradi wa Kampuni ya ujenzi wa Nyumba za Makazi, nchini Oman, Ghizlane El Gouch akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya mradi wa mkubwa wa nyumba za Makazi zinazojengwa na kampuni hiyo.

Akizungumzia maonyesho hayo kwa Dar es Salaam, Meneja Miradi wa Kampuni hiyo, Ghizlane El Gouch, amesema yataanza leo Jumatano Agosti 4, katika hoteli ya Sea Cliff Masaki kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 1 jioni.

“Tumekalimisha maonyesha haya ya kuvuatia makazi  visiwani Zanzibar na sasa ni zamu ya Dar es Salaam, ambapo maonyesho yameanza leo katika Hoteli ya Sea Cliff kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 1 jioni.

“Hivyo, tumeanza leo hadi Agosti 6 nikiwa na maana kwamba tutakuwepo hapa kwa siku tatu, timu yetu ya Muriya ina imani kuwa hafla za Dar es Saalam zitavutia wageni wengi zaidi watakaovutiwa na kupendekeza kupata fursa za uwekezaji wa mali na makazi nchini Oman.

“Baada ya kumaliza maonesho yetu hapa Tanzania timu yetu ya maonyesho itahamia nchini Kenya, hivyo niwakaribishe Watanzania mbalimbali kuchangamkia maonyesho haya,” amesema Ghizlane.

Aidha, amefafanua zaidi kuwa katika siku chache zijazo, timu ya Muriya itaonyesha maendeleo bora ya makazi na fursa za uwekezaji wa kimataifa katika maeneo yake mawili ya Jebel Sifah na Hawana Salalah, na kuzindua makazi yake mapya na eneo la burudani kwa maeneo yote mawili.

“Lengo ni kuimarisha hadhi ya nchi ya Oman kama eneo muhimu la uwekezaji wa makazi ulimwenguni, hivyo pamoja na maonyesho haya ya makazi lakini pia hafla hizo zitakwenda sambamba na kutoa mtiririko wa hotuba, mawasilisho, mazungumzo ya wataalamu ikiwamo na uchambuzi wa soko la makazi.

“Kutoka kwenye vyumba hadi majengo marefu ya kifahari (ghorofa) katika jamii zilizoendelea miradi inayotafutwa zaidi ya Muriya kote nchini Oman inaihakikishia mapato bora kuanzia dola za Marekani 133,000, hii ni pamoja na makazi ya wanunuzi na familia zao,” amesema Ghizlane.

Akizungumzia mradi wa Jebel Sifah amesema wa makazi yaliyoko umbali wa dakika 40 kutoka mji mkuu wa Muscat katika eneo la lenye ukubwa wa mita za mraba zaidi ya milioni 6.2.

“Ina nyumba za makazi, ambazo ni za kumiliki au kukodisha, sehemu za maegesho ya boti binafsi 84, sehemu za vituo vya kulia na vya kupumzika, pamoja na uwanja wa gofu uliotengezwa na Mhandisi wa viwanja vya gofu maarufu duniani, Peter Harradine.

“Jebel Sifah, ni eneo lisilokuwa na msongamano wa watu Mjini Muscat, hutoa fursa ya uwekezaji wa aina moja ya kumiliki nyumba katika eneo lililotengenezwa vizuri, pia hukupatia fursa za makazi ya kuvutia zinazokuwezesha kucheza gofu, kufanya utalii wa bahari na kuangalia milima kwa uzuri zaidi.  

Amesema pamoja na eneo la ukubwa wa mita za mraba milioni 13.6, kivutio kikuu cha makazi ya Muriya Hawana Salalah yaliyopo katika Jiji la kitropikana la Salalah katika mkoa wa Kigavana wa Dhofar, Oman.

Ameongeza kuwa yalipo makazi hayo ndipo inakopatikana hifadhi ya kwanza ya maji nchini Oman ya Hawana, maegesho ya boti binafsi 170, makazi ya bure na kumbi za rejareja, migahawa na hoteli.

“Makazi ya Hawana Salalah hulifanya eneo hili kuwa na nyumba na fursa za uwekezaji. Kila mkazi katika eneo la Hawana Salalah hufurahia mandhari nzuri ya bahari, na imejengwa kwa kuzingatia, kuangalia na kuambatana na mitindo anuwai ya maisha, saizi ya chumba kimoja au viwili vya kulala, nyumba za mijini, majengo ya kifahari yaliyotengwa peke yake na majengo ya kifahari yaliyopo pwani ya bahari.

“Pamoja na uwekezaji zaidi ya dola 750 milioni, Muriya wako nyuma ya maendeleo makubwa katika eneo la kiutawala la Sultan wa Oman na wataendelea kuleta maonesho ya makazi ambayo yanawakilisha fursa za kipekee za kuishi na uwekezaji,” amesema Ghizlane.

KUHUSU KAMPUNI YA MURIYA

Upande wake, Ofisa Mkuu wa Idara ya Fedha wa Kampuni hiyo, Mohammed Abdallah, amesema kwa kuunganisha wataalamu wa ndani na nje, Muriya ni kampuni ya ubiya kati ya msanifu anayetambulika kimataifa wa miji iliyounganishwa kikamilifu, Orascom Development Holding (ODH) (70%) na taasis ya serikali inayoongoza kwa maendeleo ya utalii nchini Oman, kampuni ya Maendeleo ya Utalii ya Oman (OMRAN) (30%).

Moja ya nyumba zinazojengwa na Kampuni ya Muriya ya nchini Oman.

“Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006, Muriya imekuwa ikiongoza uwekaji thabiti wa biashara ikijivunia uwekezaji wenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 750, katika kuendeleza Utalii Jumuishi (ITCs), wakati ikiangazia historia, urithi na uzuri wa asili wa taifa la Kisultani la Oman.

“Kupitia kampeni yao ‘Kutengeneza kesho pamoja’ kipaumbele cha Muriya ni miradi ambayo ni pamoja na, Hawana Salalah, Jebel Sifah na Kisiwa cha As Sodah, kilicho katika Bahari ya Hindi kuvuka pwani ya kusini ya Dhofar,” amesema Abdallah na kuongeza kuwa.

Eneo la makazi la Muriya la Hawana Salalah liko katika mji wa kitropikana wa Salalah katika Gavana wa Dhofar kusini mashariki mwa Oman, na eneo la mita za mraba milioni 13.6 lenye jumla ya hoteli saba, ambazo ni Fanar Hotel & Residences vyumba 577, Salalah Rotana Resort nyumba 422, Hoteli ya Boutique ya Juweira vyumba 87 na vibanda vidogo vya migahawa ya ufukweni mwa bahari 19 pamoja na nyumba ya kupumzikia wageni ya Souly Lodge ambazo zote zinafanya kazi na kufanya jumla ya vyumba vya hoteli vya kifahari vilivyopo eneo hilo kufikia hadi 1,100.

Ofisa Mkuu wa Idara ya Fedha wa Kampuni ya miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya Muriya ya nchini Oman, Mohammed Abdallah, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo Jumatano Agosti 4, 2021 wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya mradi mkubwa wa nyumba za makazi zinazojengwa na kampuni hiyo nchini Oman. Katikati ni Meneja wa Miradi wa Kampuni hiyo nchini Oman, Ghizlane El Gouch na Mshauri wa miradi hiyo, Lubna Riyami.

Makazi hayo ni nyumbani kwa hifadhi ya kwanza ya maji ya Oman ya Hawana Aqua ambapo yapo maegesho ya boti binafsi 170, makazi ya kununua au kukodi, kumbi za starehe za kukodi na migahawa.

Jebel Sifah, makazi yaliyoko dakika 40 kutoka mji mkuu wa Muscat yapo katika enelo lenye mita za mraba milioni 6.2 ambayo yamejengwa yakijumuisha hoteli tano za  ifahari zenye hadhi ya nyota tano, ambazo Hoteli ya Sifawy Boutique yenye vyumba 67 inafanya kazi.

Pia ina nyumba za makazi, ambazo zinapatikana kwa kumiliki au kukodisha, maegesho ya boti binafsi 84, na kumbi anuwai za vyakula na burudani, na uwanja wa gofu wenye mashimo 9, eneo ambalo linampa mkazi mandhari nzuri ya kuvutia ya bahari na milima ambayo ni nzuri kwa wachezaji wa mchezo wa gofu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles