22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Polisi yawashikilia viongozi sita wa BAWACHA Kagera

Renatha Kipaka, Bukoba

Viongozi sita wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA) Kagera wanashikiliwa na Jeshi la polisi kwa mahojiano kwa kosa la kuitisha mkutano uliokuwa ukishinikiza kuachiwa huru Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Kauli hiyo imetolewa na leo Agosti 4, 2021 na Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Kagera, Revokatus Malimi wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari.

Malimi amesema viongozi hao wamekamatwa leo wakiwa Katika maandarizi ya Mkutano huo.

Hata hivyo Kamanda huyo amesema kuwa jambo lolote linapofikishwa mahakamani haliruhusiwi kujadiliwa sehemu yoyote tofauti na mahakamani.

“Nitumie nafasi hii kutoa onyo kuwa Jeshi la polisi halitamvumilia mtu yeyote atakae jaribu kuvuruga amani, sheria utachukuwa mkondo wake,”amesema Malimi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles