Na Winfrida Mtoi
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohammed Dewji(MO) leo Julai 30.202, amekabidhi sh 20 billioni za uwekezaji katika asilimia 49 ya hisa anazopewa naklabu hiyo katika mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu baada ya mchakato kukamilika.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi mfano wa hundi, jijini Dar es Salaam, MO amesema katika kipindi cha miaka minne alichokuwa na Simba, ametoa fedha zaidi ya hizo lakini kuna watu wanamsema kuwa hana fedha.
“Mimi kwenye miaka minne nimewekeza sh bilioni 21.3 na kila pesa ambayo nimetoa ni kwa kutaka mafanikio na kila mwaka nimetoa si chini ya bilioni 5.3, hizi ni pesa za ziada kwa sababu napenda Simba, lakini kitu kinachoniumiza ni watu kusema MO hana bilioni 20,” amesema.
Ameeleza kuwa mabadiliko yamekamili na kuna vipengere lazima vikamilishwe ambayo ni kutoa fedha zinazotakiwa na amezitoa rasmi.
“Mjue sasa kwamba sinunui hisa asilimia 49 kwa bilioni 19.6, inaweza kufika bilioni 43 au 44 ambayo imezidi kutokana na thamani ya klabu kupanda na imezidi kutokana na uwekezaji.
“Simba ndiyo imeweka mpira wa Tanzania katika ramani ya Afrika, tumetoa timu nne na wenzetu wananufaika na sisi tumefikia malengo yetu,” ameeleza.